MIFUKO YA JAMII YATAKIWA KUSHIRIKIANA NA BMT KUHAMASISHA USHIRIKI WA WANAWAKE KATIKA MICHEZO

Na; Mwandishi Maalum
Makamu wa Rais, Mhe. Samia Suluhu ameitaka Mifuko ya Hifadhi ya Jamii nchini kushirikiana na Baraza la Michezo la Taifa (BMT) kuandaa program mbalimbali za kuhamasisha ushiriki wa wanawake katika michezo na mazoezi ya viungo ili kuweza kuondoa mila potofu zinazo wakandamiza wanawake katika ushiriki wa michezo na mazoezi ya viungo.

PICHA NO. 2
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera , Bunge , Ajira na Watu wenye ulemavu), Jenista Mhagama akishiriki mazoezi ya viungo (wa pili kulia), wengine ni wajumbe wa BMT wakati wa tamasha la michezo la kusherekea siku ya Wanawake Duniani katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam lililoandaliwa na Baraza la Michezo la Taifa tarehe 05 Machi, 2016.

Amesema hayo katika hotuba yake iliyosomwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia, (Sera, Bunge, Ajira, na Watu wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama (Mb) katika Tamasha la michezo la kusherekea siku ya wanawake Duniani lililofanyika katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam leo tarehe 05 Machi, 2016.

maadhimishombiro
Mkuu wa Wilaya, Mjumbe wa Baraza na Mwanamichezo mahiri Bibi. Zainab Mbussi (mwenye trakisuti ya bluu) akiongoza mazoezi katika kusherekea siku ya wanawake duniani iliyofanyika katika uwanja wa uhuru Tar. 05 Machi 2016 jijini Dar-es-salaam.
maadhimisho jenifa
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera , Bunge , Ajira na Watu wenye ulemavu), Jenista Mhagama akishiriki mazoezi ya viungo (wa pili kulia), wengine ni wajumbe wa BMT wakati wa tamasha la michezo la kusherekea siku ya Wanawake Duniani katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam lililoandaliwa na Baraza la Michezo la Taifa tarehe 05 Machi, 2016.

“Wanawake tunaweza kuwa mhimili imara katika kuleta maendeleo ya jamii yetu kwa kuwa tunaweza katika elimu, siasa, uchumi na michezo pia. Pamoja na majukumu aliyonayo mwanamke katika familia, Changamoto tuliyonayo ni kutokuwepo elimu ya kutosha juu ya faida ya mwanamke kushiriki katika michezo na unyanyasaji wa jinsia kwa mwanamke katika ushiriki wa michezo. Hivyo basi, sekta binafsi, makampuni taasisi, mifuko ya Hifadhi ya Jamii na watu binafsi washirikiane na BMT nataka mtusaidie kudhamini michezo na mazoezi ya viungo ya wanawake” alisema.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Uratibu na Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye ulemavu Mhe. Jenista Mhagama (wapili kushoto) akipata maelekezo kuhusu michezo mbalimbali iliyoandaliwa kutoka kwa Kaimu Katibu Mtendaji Baraza la Michezo la Taifa Bw. Mohamed Kiganja (wapili kulia) wakati wa tamasha la maadhimisho kuelekea kilele cha siku ya wanawake katika viwanja vya Uhuru leo jijini Dar es Salaam.

Mhagama aliongeza kuwa wanawake kama walezi wa familia wakiwa na mazoezi ya viungo itasaidia kuwashawishi wanafamilia kuwa wanamazoezi hivyo kuifanya familia kufaidika na ushiriki huo kwa kuwa familia yenye afya, upendo, amani na ushirikiano na hatimaye kujenga taifa imara linaloweza kuzalisha uchumi endelevu.

maadhimisho2

“Mifuko ya Hifadhi mkihamasisha watu kushiriki katika jamii hasa wanawake, watoto na watu wenye ulemavu, taifa letu litakuwa na watu wenye Afya hivyo mifuko hii kama Mfuko wa Bima ya Afya ikihamasisha michezo, itapunguza gharama kubwa wanazotumia kutibu wananchama wake wenye magonjwa yasiyo ya kuambukiza ili kuwezesha wananchi wenye afya bora kushiriki kikamilifu katika shughuli za maendeleo” Alisisitiza Mhagama.

Awali akimkaribisha katika Tamasha hilo, Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Michezo la Taifa, Zainabu Vulu alisema kuwa pamoja na jitihada zinazofanywa na Baraza hilo za kuhamasisha ushiriki wa wanawake katika michezo lakini changaomoto kubwa inayowakabili ni viwanja vingi vya wazi vya michezo vimevamiwa na kuendelezwa kwa shughuli ambazo sio za kuendeleza michezo.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Uratibu na Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akirusha mpira kuashiria ufunguzi wa mchezo wa mpira wa pete wakati wa tamasha la maadhimisho kuelekea kilele cha siku ya wanawake katika viwanja vya Uhuru leo jijini Dar es Salaam. Anayezuia mpira ni Mjumbe wa Baraza la Michezo ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Rungwe Bibi. Zainabu Mbussi.

“Tunawahamasisha wanawake washiriki katika michezo na mazoezi ya viungo lakini viwanja vingi vilivyo karibu na maeneo yao wanayo ishi yamevamiwa hali ambayo huwapa tabu wanawake wengi kushiriki kwa kuzingatia majukumu waliyonayo katika familia, tunaomba uwaagize Wizara ya Ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi pamoja na serikali ya mitaa kuhakikisha maeneo ya viwanja vya michezo hivyo vinarudishwa katika hali yake ya mwanzo ili wanawake na wasichana washiriki katika mazingira salama ” alisema Vulu.

maadhimisho3

Tamasha hilo liloandaliwa na Baraza la Michezo la Taifa kwa lengo la kusherehekea Siku ya Wanawake Duniani ambayo huadhimishwa kila mwaka mwezi Machi 8, liliwashikisha washiriki kutoka shule za wasichana za jijini Dar es Salaam, Kikosi cha Maadhimisho, Vyama na mashirikisho ya michezo, Timu za wanawake za mpira wa miguu na mpira wa pete za wilayani Temeke, Makongo na za Jeshi la Wananchi pamoja na wadau wa michezo nchini; lilikuwa na kauli mbiu;

“50/50 ifikapo 2030 tuongeze jitihada; “maendeleo ya wanawake kupitia michezo yanawezekana”

260 total views, 1 views today

Fuatilia Mchezo, like:
0

Leave a Reply

Michezo ni yetu wote, fuatilia, Wataarifu wengi

Follow by Email4
Facebook
Facebook
YouTube0
YouTube
Google+0
Google+
http://nationalsportscouncil.go.tz/blog/2016/03/05/mifuko-ya-jamii-yatakiwa-kushirikiana-na-bmt-kuhamasisha-ushiriki-wa-wanawake-katika-michezo/">
RSS