WACHEZAJI WA MPIRA WA MAGONGO WATAKIWA KUJITUMA ILI KUILETEA SIFA NCHI.

Wachezaji wa mpira wa Magongo (Twende Hockey) wametakiwa kujituma na kuiletea sifa nchi katika mashindano yao ya kufuzu kombe la Afrika yanayotarajia kufanyika Machi 18 hadi 28 mwaka huu nchini Namibia.

Rai hiyo imetolewa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye wakati wa kukabidhi bendera kwa timu hiyo leo jijini Dar es Salaam.

“Nawatakia mafanikio katika mashindano hayo, muwe na moyo wa kushinda siyo kushiriki, na nawaahidi kuwapokea mkirudi na ushindi“alisema Mhe. Nnauye”.

Aidha, Mhe. Nnauye amesema kuwa Serikali itakuwa karibu na Vyama/Mashirikisho ya michezo ili kuhakikisha kuwa michezo yote inafanya vizuri kwa lengo la kuitangaza na kuiletea sifa nchi yetu.

Waziri Nnauye aliwaomba NMB na wadhamini wengine kusaini mikataba ya muda mrefu kwani matokeo mazuri hupatikana kwa kuwekeza kwa muda, vilevile aliwataka wadhamini kudhamini michezo yote na siyo soka pekee.

Kwa upande wake Afisa fedha Mkuu kutoka NMB Bw. Waziri Barnabas alisema kuwa NMB imekuwa ikidhamini mchezo huo kwa miaka miwili sasa na michezo mingine, ambapo aliwataka wanamichezo kuwa na ari ya kuleta ushindi na sifa kwa Taifa kuwafanya wadhamini kuwa na moyo wa kudhamini zaidi.

Awali Mwenyekiti wa Chama cha Mchezo wa mpira wa Magongo Bw. Abraham Sykes, alisema mchezo huo ulisahaulika ila anaamini kuwa vijana wake wameandaliwa vyema hivyo watafanya na wataendelea kufanya vizuri.

Timu ya Mpira wa Magongo inatarajia kuondoka nchini tarehe 13 Machi mwaka huu kuelekea nchini Namibia kwa mashindano hayo, ambapo NMB wamewakabidhi hundi ya Sh.milioni 25 na mabegi ya kuweka vifaa vya mchezo huo.

60 total views, 1 views today

Fuatilia Mchezo, like:
0

Leave a Reply

Michezo ni yetu wote, fuatilia, Wataarifu wengi

Follow by Email14
Facebook
Facebook
YouTube0
YouTube
Google+0
Google+
http://nationalsportscouncil.go.tz/blog/2016/03/09/wachezaji-wa-mpira-wa-magongo-watakiwa-kujituma-ili-kuiletea-sifa-nchi/">
RSS