KATIBU MKUU WA BMT APANGA MIKAKATI NA WAFANYAKAZI KUENDELEZA MICHEZO NCHINI

Na. Mwandishi wetu

Kaimu Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Bw. Mohamed Kiganja amesema, atafanya vikao vya mara kwa mara na Wafanyakazi wa Baraza  ili kupanga mikakati ya kuendeleza sekta ya michezo nchini.

Rai hiyo ameitoa leo katika kikao chake na wafanyakazi wa Baraza ambacho ni cha pili tangu ateuliwe 17 Januari, mwaka huu.

ktb2
Kaimu Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Bw. Mohamed Kiganja (aliyevaa tai) akitoa maelekezo kwa Wafanyakazi wa Baraza wakati wa kikao tarehe 16 Machi, 2016.

Aliendelea  kuwa, hatuna buni kukutana mara kwa mara ili kupanga mikakati yenye kuleta maendeleo katika sekta ya Michezo nchini kwetu.

Alisisitiza kuwa kila Mfanyakazi ahakikishe anawajibika katika majukumu yake na hatuna budi  wabunifu ili tuinue Baraza na sekta hii huku akiwataka Maafisa Michezo kuelewa michezo ni mtambuka hivyo hawana budi kutafuta wadau wa kufanya kazi na Baraza ili kuinua sekta ya michezo nchini.

katbu4

Aliendelea kuwa Ofisi ya fedha nao wawe wabunifu wa kutafuta  vyanzo vya mapato kulifanya Baraza liweze kujiendesha bila kutegemea ruzuku ya Serikali pekee,  wakati Maafisa Utawala na Utumishi wakitakiwa kuhakikisha njia za kuwasaidia Wafanyakazi kwenda kwenye kozi na mafunzo tofauti ili kuleta tija katika utendaji wao.

Katibu Mkuu alihitimisha kwa kusisitiza wafanyakazi kujituma katika majukumu yao.

 ktb3

 

 

49 total views, 1 views today

Fuatilia Mchezo, like:
0

Leave a Reply

Michezo ni yetu wote, fuatilia, Wataarifu wengi

Follow by Email14
Facebook
Facebook
YouTube0
YouTube
Google+0
Google+
http://nationalsportscouncil.go.tz/blog/2016/03/16/katibu-mkuu-wa-bmt-apanga-mikakati-na-wafanyakazi-kuendeleza-michezo-nchini/">
RSS