BARAZA LA MICHEZO LA TAIFA (BMT) NA MIKAKATI YA KUINUA SEKTA YA MICHEZO NCHINI.

Baraza la Michezo la Taifa kwa kushirikiana na Taasisi binafsi ya ‘Pro event masters limited’ wataendesha Semina ya Masoko na Udhamini katika michezo (Sports Marketing and Sponsorship), Semina inatarajiwa kuwa ya siku tatu (3) kuanzia tarehe 14 hadi 16 Aprili, 2016  katika Ukumbi  wa Uwanja wa Taifa.

mafunzo2
Kaimu Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo la Taifa Bw. Mohamed Kiganja akifafanua jambo kwa Waandishi (hawapo pichani) leo katika Ukumbi wa Baraza.

Akizungumza katika mkutano na Waandishi wa habari leo asubuhi, Kaimu Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo la Taifa alieleza kuwa, Baraza limeamua kuendesha Semina hiyo, baada ya kubaini uwepo wa changamoto kubwa ya upatikanaji wa rasilimali muhimu za uendeshaji wa michezo, ikiwemo rasilimali fedha na vifaa kwa Vyama vyetu vya Michezo.

Aliendelea kuwa Semina hiyo inategemewa kuwa ya mpango wa muda mfupi katika kuvipatia uwezo Vyama vyetu kujiendesha, huku akisisitiza kuwa  Baraza pia litaandaa mipango mikakati ya Semina ya muda wa kati na muda mrefu katika kupata ufumbuzi wa kuendeleza michezo nchini.

Kaimu Katibu Mkuu alifafanua kuwa kila mshiriki atawajibika kuchangia shilingi za kitanzania laki mbili na nusu (250,000) ili kufanikisha semina hiyo.

Aidha, Baraza  linatarajia Vyama vyote na Mashirikisho yote ya Michezo na wadau wengine kujitokeza kushiriki katika Semina hiyo muhimu kwa maendeleo ya michezo nchini, “alisema Kiganja”.

Awali Mkurugenzi wa Kampuni ‘Pro event masters limited’ Bw. Henry Tandau alieleza kuwa wataendelea kufanya kazi na Baraza kwa kuendesha semina za muda mfupi, wa kati na mrefu kwa Vyama, Mashirikisho na wadau wote wa michezo   kuhakikisha michezo nchini inafika mahali pazuri.

mafunzo3
Mkurugenzi wa Pro event masters ltd Henry Tandau akieleza kwa Waandishi (hawapo pichani) jinsi Kampuni yao itakavyofanya kazi na Baraza kuinua sekta ya Michezo

Aliongeza kuwa, Taasisi yao inajihusisha na masuala ya Uendeshaji wa Matukio, Ushauri na Mafunzo mbalimbali ya michezo.

Waalikwa wa semina hiyo ni  pamoja na wadau wa michezo toka Makampuni mbalimbali ikiwemo, TIGO, AIRTEL, ZANTEL, NMB, VODACOM,  NSSF PPF, PSPF, S.S. BAHRESSA AND COMPANY (AZAM), GEITA GOLD MINE, NBC, TBL, COCA-COLA, FNB, BOA BANK, PEPSI, TTB, TICS, NESFAL, na SYMBION.

Kiganja alihimisha kwa kusema kuwa, “ELIMU NI GHARAMA”Kila mshiriki atawajibika kulipa ada hiyo ili apate ridhaa ya kuhudhuria mafunzo hayo.  Fedha hizi zitasaidia katika uendeshaji wa mafunzo hayo kwa kutoa chai, maji, chakula, vyeti na gharama za elimu.

149 total views, 1 views today

Fuatilia Mchezo, like:
0

Leave a Reply

Michezo ni yetu wote, fuatilia, Wataarifu wengi

Follow by Email5
Facebook
Facebook
YouTube0
YouTube
Google+0
Google+
http://nationalsportscouncil.go.tz/blog/2016/03/17/baraza-la-michezo-la-taifa-bmt-na-mikakati-ya-kuinua-sekta-ya-michezo-nchini/">
RSS