TWIGA STARS WATAKIWA KUWAPA RAHA WATANZANIA

Kaimu Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Mohamed Kiganja amewataka Wachezaji wa Timu ya Taifa ya Wanawakekuwapa raha watanzania kwa kuhakikisha wanashinda mchezo wao wa marudiano na Timu ya Taifa ya Wanawake ya Zimbabwe inayotarajiwa kuchezwa Jumapili Machi 20.

ongea
Kaimu Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Mohamed Kiganja akisisitiza jambo kwa wachezaji wa Timu ya Taifa ya Wanawake ya Mpira wa Miguu , “Twiga Stars”, wakati wa zoezi la kuikabidhi bendera timu hiyo tarehe 18 Machi , 2016 Jijini Dar es Salaam, kwa ajili ya mchezo wa marudiano na Timu ya Taifa ya Wanawake ya Zimbabwe inayotarajiwa kuchezwa Jumapili Machi 20, 2016.

Akiongea wakati wa zoezi la kuikabidhi bendera timu hiyo tarehe 18 Machi , 2016 lililofanyika katika Ofisi za TFF Jijini Dar es Salaam, alieleza kuwa watanzania wanayo imani kubwa na timu hiyo hivyo ni jukumu lao kuhakikisha wanashinda mchezo huo.
“Mnapoondoka leo kuelekea Zimbabwe mwende mkifikiria mambo matatu, kuitendea haki nchi yenu, kuutendea haki mpira na kuitendea haki Timu ya Taifa ya Wanawake Kwenye mchezo wenu wachezaji lazima mpendane, mcheze kwa kutumia nguvu na mfikirie kuiletea nchi sifa.” alisema Kiganja.

 Kocha wa Timu ya Taifa ya Wanawake ya mpira wa miguu, Nasra Mohamed akieleza jambo wakati wa zoezi la kuikabidhi bendera timu hiyo tarehe 18 Machi , 2016 Jijini Dar es Salaam, kwa ajili ya mchezo wa marudiano na Timu ya Taifa ya Wanawake ya Zimbabwe inayotarajiwa kuchezwa Jumapili Machi 20, 2016.

Kwa upande wake Kocha wa Timu ya Taifa ya Wanawake ya mpira wa miguu Nasra Mohamed alibainisha kuwa, wachezaji wameandaliwa vyema na mahitaji yao yote yako kamili
“Timu yangu ushindi wa ugenini ni muhimu sana na tayari tumeshayafanyia marekebisho makosa yaliyojitoleza katika mchezo wetu wa awali hivyo wachezaji wangu wameandaliwa vyema kiufundi na kisaikolojia kwa ajili ya kuwapa raha watanzaniai” alisema Mohamed

nahonda
Nahodha wa Timu ya Taifa ya Wanawake ya mpira wa miguu, Asha Rashidi akieleza jambo wakati wa zoezi la kuikabidhi bendera timu hiyo tarehe 18 Machi , 2016 Jijini Dar es Salaam, kwa ajili ya mchezo wa marudiano na Timu ya Taifa ya Wanawake ya Zimbabwe inayotarajiwa kuchezwa Jumapili Machi 20, 2016.

Timu hiyo itaondoka na wachezaji 19, pamoja na Viongozi sita. Ikiwa na kumbukumbu za kupoteza mchezo wa awali kwa kufungwa goli 2 dhidi ya goli 1, katika uwanja wa Chamazi jijini Dar es Salaam.

Kaimu Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Mohamed Kiganja (katikati walio kaa) akiwa na wachezaji wa Timu ya Taifa ya Wanawake ya Mpira wa Miguu , “Twiga Stars”, mara baada ya kukabidhi bendera timu hiyo tarehe 18 Machi , 2016 Jijini Dar es Salaam, kwa ajili ya mchezo wa marudiano na Timu ya Taifa ya Wanawake ya Zimbabwe inayotarajiwa kuchezwa Jumapili Machi 20, 2016.

MWISHO

133 total views, 2 views today

Fuatilia Mchezo, like:
0

Leave a Reply

Michezo ni yetu wote, fuatilia, Wataarifu wengi

Follow by Email5
Facebook
Facebook
YouTube0
YouTube
Google+0
Google+
http://nationalsportscouncil.go.tz/blog/2016/03/18/twiga-stars-watakiwa-kuwapa-raha-watanzania/">
RSS