TWIGA YAREJEA KWA SARE NA MIGHTY WARRIORS.

Timu ya Taifa ya Wanawake Tanzania ya Mpira wa Miguu ‘Twiga Stars’ imerejea nyumbani kwa sare ya bao 1-1 dhidi ya wenyeji Zimbabwe ‘Mighty Warriors’ katika mchezo uliochezwa jana jioni katika uwanja wa Rufaro jijini Harare.

Twiga katika mchezo wao imecheza vizuri na kuweza kuwabana wenyeji katika uwanja wao wa nyumbani kwa kuwalazimisha sare, hata hivyo weyeji kupata nafasi ya kusonga mbele katika hatua inayofuata kwa jumla ya mabao 3-2.

Kwa matokeo hayo Twiga Stars imetolewa kwenye michuano ya kuwania kufuzu kwa Fainali za Mataifa ya Afrika kwa Wanawake zitakazofanyika mwishoni mwa mwaka huu nchini Cameroon.

Kikosi cha Twiga Stars kimerejea nyumbani jioni ya leo kwa usafiri wa shirika la ndege la Fastjet.

36 total views, 1 views today

Fuatilia Mchezo, like:
0

Leave a Reply

Michezo ni yetu wote, fuatilia, Wataarifu wengi

Follow by Email14
Facebook
Facebook
YouTube0
YouTube
Google+0
Google+
http://nationalsportscouncil.go.tz/blog/2016/03/21/twiga-yarejea-kwa-sare-na-mighty-warriors/">
RSS