KAIMU KATIBU MKUU WA BMT ATETA NA VIONGOZI WAKUU WA TOC.

Kaimu Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Bw. Mohamed Kiganja amekutana na baadhi ya Viongozi wa Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC) na kufanya mazungumzo nao kuhusu namna ya kufanya kazi kwa ushirikiano wa karibu baina ya Taasisi hizo, kikao kilichofanyika katika Ukumbi wa Baraza tarehe 24 Machi, mwaka huu.

toc2

Katibu wa Baraza alifafanua kuwa Taasisi hizo hazina budi kufanya kazi kwa pamoja kwa kufanya mafunzo ya Kuongoza, Kutawala na Ukocha pamoja na kuanzisha kozi mbalimbali kwa Vyama/Mashirikisho ili kuinua sekta ya Michezo kwa faida ya Watanzania.

“Tusahau tulikotoka tufungue milango upya kwa kuimarisha utendaji wetu, mawasiliano na tufanye vikao vya mara kwa mara ili kujenga uhusiano wetu kwa maendeleo ya michezo ya Taifa letu, alisisitiza Kiganja”.

toc3

Kwa upande wake Rais wa TOC Bw. Gulam A. Rashid, ‘alisema kuwa azimio la kikao hicho liwe ni kuunganisha nguvu yetu kwa pamoja kati ya TOC na BMT katika kuwaletea Mafunzo mbalimbali ya maendeleo Vyama na Mashirikisho ya Michezo nchini.

toc4

Naye Katibu Mkuu wa Kamati ya Oliympiki Tanzania Bw. Filbert Bayi alijibu agenda iliyohusu, hatma ya timu za Tanzania kwenye Michezo ya RIO 2016, kuwa timu ziko kwenye maandalizi na hatma ya timu shiriki itajulikana mwisho wa mwezi wa Tano, ambapo timu itakayokidhi vigezo ndiyo itakayoshiki mashindano hayo.

Kaimu Katibu Mkuu alihitimisha kikao kwa kuwataka TOC kuyafanyia kazi maazimio ya kikao huku akiwaahidi kuwasaidia sehemu yoyote wanapotaka kufanya kazi ya kimichezo nchini

toc1

169 total views, 1 views today

Fuatilia Mchezo, like:
0

Leave a Reply

Michezo ni yetu wote, fuatilia, Wataarifu wengi

Follow by Email5
Facebook
Facebook
YouTube0
YouTube
Google+0
Google+
http://nationalsportscouncil.go.tz/blog/2016/03/24/kaimu-katibu-mkuu-wa-bmt-ateta-na-viongozi-wakuu-wa-toc/">
RSS