KAIMU KATIBU MKUU WA BMT AKUTANA NA VIONGOZI WA TPBC

Kaimu Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Bw. Mohamed Kiganja amekutana na Viongozi wa Kamisheni ya ngumi za kulipwa Tanzania na kufanya mazungumzo nao kuhusu mikakati ya Kamisheni hiyo katika kuinua mchezo huo, hayo yamefanyika leo katika Ukumbi wa BMT.

“BMT ndio chombo pekee cha Serikari kinachosimamia michezo nchini, hivyo ni wajibu wa Baraza kukutana na viongozi wa Vyama na Mashirikisho kuona wanamikakati ipi kuendeleza michezo, alisema Kiganja”.

Kaimu Katibu Mkuu akifafanua jambo kwa wajumbe wakati wa kikao, kulia ni Afisa Michezo ambaye ndiye deski Ofisa wa Kamisheni hiyo, Apansia Lema
Kaimu Katibu Mkuu akifafanua jambo kwa wajumbe wakati wa kikao, kulia ni Afisa Michezo ambaye ndiye deski Ofisa wa Kamisheni hiyo, Apansia Lema

Aliendelea kuwa usajili wa Chama/Shirikisho au Taasisi yoyote inayojihusisha na michezo unatakiwa kufanyika Baraza la Michezo la Taifa (BMT) kama sheria inavyoelekeza, na Msajili atakuwa Baraza kuanzia mwezi Julai mwaka huu siyo Wizarani tena.

Aidha, Kampuni zingine zinazojihusisha na mchezo huu ni lazima ziwajibike kwa Kamisheni ya ngumi za kulipwa Tanzania (TPBC) kwani ndio Taasisi pekee iliyosajiliwa kusimamia mchezo huu kabla kuja Baraza kwa taratibu zingine.

Rais wa Kamisheni ya ngumi za kulipwa Tanzania (TPBC) alieleza baadhi ya changamoto wanazokabiliana nazo kwa Kaimu Katibu Mkuu wa BMT (hayupo pichani) kushoto ni Mweka Hazina wa TPBC Joe A. Joseph katika kikao hicho tarehe 30 Machi, 2016.

TPBC mnajukumu kubwa la kuisaidia Serikali katika kusimamia ngumi za kulipwa Tanzania “alisisitiza Kiganja”.

Kwa upande wake Rais wa Kamisheni ya ngumi za kulipwa Tanzania Bw. Chaurembo Palasa alieleza kuwa, Kamisheni yao ina changamoto nyingi pamoja na kupewa jukumu la kusimamia ngumi za kulipwa Tanzania kwakuwa Taasisi zingine hazina ushirikiano na hazifuati katiba na taratibu za TPBC.

Viongozi wa Kamisheni ya ngumi za kulipwa Tanzania (TPBC) wakiwa makini kumsikiliza Kaimu Katibu Mkuu wa BMT Bw. Kiganja wakati wa kikao nao leo tarehe 30 Machi, 2016 katika Ukumbi wa Baraza.
Viongozi wa Kamisheni ya ngumi za kulipwa Tanzania (TPBC) wakiwa makini kumsikiliza Kaimu Katibu Mkuu wa BMT Bw. Kiganja wakati wa kikao nao leo tarehe 30 Machi, 2016 katika Ukumbi wa Baraza.

Kaimu Katibu Mkuu alisema kuwa kila Chama/Shirikisho kuanzia Julai wanatakiwa kuleta katiba zao zipitiwe na kufanyiwa maboresho ili kuwe na Katiba imara yenye kutekelezeka kwa Msimamizi na anayesimamiwa.

Aliongeza kuwa anatarajia kuwa na kikao cha pamoja kati ya TPBC na Taasisi zote zilizosajiliwa na zinazojihusisha na mchezo wa ngumi za kulipwa wiki ijayo.

Kikao kilimhusisha Kaimu Katibu Mkuu wa BMT Bw. Mohamed Kiganja, Maafisa Michezo wa Baraza, Benson Chacha, Halima Bushiri na Apansia Lema, Viongozi wa TPBC akiwemo, Rais Bw. Chaurembo Palasa, Katibu Mkuu Hamis Kimanga, Joe Joseph, Ally Bakari,Buchato Ndana na Fidel Haynes.

31 total views, 1 views today

Fuatilia Mchezo, like:
0

Leave a Reply

Michezo ni yetu wote, fuatilia, Wataarifu wengi

Follow by Email14
Facebook
Facebook
YouTube0
YouTube
Google+0
Google+
http://nationalsportscouncil.go.tz/blog/2016/03/30/kaimu-katibu-mkuu-wa-bmt-akutana-na-viongozi-wa-tpbc/">
RSS