BMT YAAGIZWA KUFUATILIA VIWANJA VYA MICHEZO VILIVYOVAMIWA NA KUVIREJESHA KWA JAMII KWA AJILI YA MATUMIZI YA MICHEZO.

Agizo hilo limetolewa leo na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Annastazia James Wambura alipofanya ziara katika ofisi za Baraza hilo kwa ajili ya kuona utendaji na changamoto zinazolikabili baraza hilo.

naibu1
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sana na Michezo Mhe. Annastazia James Wambura akipokelewa na Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Mohamed Kiganja alipofanya Ziara katika ofisi za Baraza hilo leo jijini Dar es Salaam. Kulia kwake ni mjumbe wa BMT Bibi. Jenifer Mmasi Shang’a na Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo Makoye Alex Nkenyenge

Mhe. Wambura alisema kuwa kumekuwa na changamoto ya maeneo mengi yaliyotengwa kwa shughuli za kijamii ikiwemo michezo kuvamiwa na watu na kufanya shughuli nyingine kinyume na taratibu.
“Kama ilivyo katika Ilani ya uchaguzi BMT mnawajibika kufuatilia maeneo yote yaliyotengwa kwa ajili ya shughuli za michezo fuatilieni kwa karibu kikiwemo kile cha Tandika ambacho tulikwisha anza nacho” Alisema Naibu Waziri.

naibu2
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sana na Michezo Bibi. Nuru Halfani Mrisho Milao akieleza jambo kwa wafanyakazi wa BMT wakati wa ziara ya Naibu Waziri wa wizara hiyo Mhe. Annastazia James Wambura (katikati) katika ofisi za Baraza la Taifa la Michezo leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Katibu Mkuu wa BMT Mohamed Kiganja.


Aidha Wambura alihimiza Bmt kuhakikisha inahamasisha ushiriki wa wanawake katika michezo kwa kuwa michezo ipo kwa ajili ya wote na kuongeza kuwa mbali na mashindano michezo pia hujenga afya ya mwanadamu, ni ajira na huleta na kuimarisha mahusiano kwa jamii.

naibu4
Katibu Mkuu wa BMT Mohamed Kiganja akifafanua jambo mbele ya Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Annastazia James Wambura (kushoto) alipofanya ziara katika ofisi za Baraza hilo leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Afisa Utumishi wa BMT Bw. Jacob Nduye na wapili kulia ni mjumbe wa BMT Bibi. Jenifer Mmasi Shang’a


Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Mohamed Kiganja alisema kuwa pamoja na changamoto zilizopo watahakikisha wanapiga hatua katika kukuza sekta ya michezo kwani BMT ndiyo mkono pekee wenye dhamana ya kusimamia michezo nchini kisheria.
Awali alieleza changamoto zinazowakabili katika kutekeleza majukumu yao kuwa ni kutokuwa na Ofisi ya kudumu, Sheria kupitwa na wakati, ufinyu wa bajeti, upungufu wa wafanyakazi na hasa Maafisa Michezo, mwingiliano wa Wizara mbili katika utekelezaji katika ngazi ya Manispaa na Halmashauri Maafisa Michezo wanawajibika chini ya Wizara ya TAMISEMI hivyo kuna haja ya kukaa pamoja na kuangalia namna bora ya kushirikiana.
Naibu Katibu Mkuu Nuru Khalifan aliyeambatana naye katika ziara hiyo alisema kuwa, atazifanyia kazi changamoto walizomweleza Naibu Waziri kama itakavyowezekana kwakuwa ndiye mtendaji.

naibu6
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sana na Michezo Mhe. Annastazia James Wambura akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa BMT leo jijini Dar.Kutoka kushoto waliokaa ni Naibu Katibu Mkuu wa wizara hiyo na wa mwisho kulia waliokaa ni Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Mohamed Kiganja.


Mwisho>

31 total views, 1 views today

Fuatilia Mchezo, like:
0

Leave a Reply

Michezo ni yetu wote, fuatilia, Wataarifu wengi

Follow by Email14
Facebook
Facebook
YouTube0
YouTube
Google+0
Google+
http://nationalsportscouncil.go.tz/blog/2016/04/05/bmt-yaagizwa-kufuatilia-viwanja-vya-michezo-vilivyovamiwa-na-kuvirejesha-kwa-jamii-kwa-ajili-ya-matumizi-ya-michezo/">
RSS