NAPE: ITUMIENI MICHEZO KUJENGA UZALENDO NA KULETA SIFA KWA TAIFA.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mheshimiwa Nape Moses Nnauye amelitaka Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kujenga uzalendo na kuiletea nchi sifa kupitia michezo.

Rai hiyo ameitoa wakati wa makabidhiano ya Ulingo wa Kimataifa wa ngumi kwa Jeshi hilo ili wautumie kujiandaaa vyema katika mashindano mbalimbali ya kitaifa na kimataifa huku akisisitiza kuwa anaamini ni sehemu salama na wana nidhamu ya kuutunza.

“Jeshi la wananchi wa Tanzania (JWTZ) limekuwa na mchango mkubwa sana katika michezo na kuiletea sifa nchi katika mashindano mbalimbali ya majeshi,  hivyo hatukuwa na shaka tulipoletewa ombi la Ulingo huu na kuwataka wautumie vyema na kuleta heshima nchini, “alieleza Nape”.

nape1

Aidha, Waziri nape alieleza kuwa Wizara yake itaendelea kutoa ushirikiano kwa jeshi katika michezo yote na kuwataka baraza la michezo ya majeshi (BAMMATA) kurudisha michezo majeshini kwakuwa inajenga uzalendo na kuimarisha umoja, undugu na urafiki.

Kwa upande wake Mkuu wa mafunzo na oparesheni jeshini Meja Generali Issa Nassor alimshukuru Waziri Nape na Wizara kwa ujumla kwa kuona umuhimu wa kuwapatia ulingo huo na kusema kuwa utawasaidia sana katika mazoezi na mashindano mbalimbali.

“Ulingo huu utatumika kwa mabondia wote Tanzania kwani utajenga umoja na kukuza mchezo huo na naahidi kushirikiana na askari wote kwakuwa michezo ni sehemu ya kazi pia’ “ alisema Meja Generali Issa”.

Aliongeza kuwa, ulingo waliopewa ni chachu ya mazoezi na itawajengea mabondia  moyo wa ushindi na kuwataka wadau mbalimbali wa michezo kuunga mkono jitihada za jeshi hilo kwani wana nia yakuwa kituo bora cha michezo ikizingatiwa jeshi ni kioo cha Taifa.

Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo imetoa ulingo huo wa kimataifa kwa jeshi hilo ikiwa ni msaada waliopewa na Serikali ya watu wa China mwaka ili kuboresha mchezo wa masumbwi nchini.

nape2

46 total views, 1 views today

Fuatilia Mchezo, like:
0

Leave a Reply

Michezo ni yetu wote, fuatilia, Wataarifu wengi

Follow by Email14
Facebook
Facebook
YouTube0
YouTube
Google+0
Google+
http://nationalsportscouncil.go.tz/blog/2016/04/08/nape-itumieni-michezo-kujenga-uzalendo-na-kuleta-sifa-kwa-taifa/">
RSS