BMT YAIAGIZA TFF KUHAKIKISHA KLABU YA YANGA INAFANYA UCHAGUZI

Kaimu Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Bw. Mohaned Kiganja  ameliagiza Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF)  kuhakikisha Klabu ya Yanga inafanya  Uchaguzi  ndani ya muda usiozidi  Juni 30 mwaka huu.

DSC05987
Kaimu Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Bw. Mohamed Kiganja akiongea mbele ya waandishi wa habari hawapo pichani katika mkutano uliofanyika leo jijini Dar es salaam.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Rai hiyo ameitoa leo  katika mkutano na Waandishi wa Habari  akirejea kikao alichokaa na Uongozi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF),  Uongozi  wa  Chama cha mpira wa miguu Mkoa wa Dar es salaam (DRFA) pamoja na Msajili Msaidizi wa Vyama na Vilabu vya Wilaya ya Ilala wakizungumzia hatma ya uchaguzi wa Klabu hiyo, kikao kilichokaliwa tarehe 18 mwezi huu Jijini Dar es salaam.

Alifafanua kuwa,  Klabu ya Yanga ilipewa maelekezo na TFF katika mkutano uliofanyika tarehe 1 Juni, 2014 uliomwingiza Mwenyekiti aliyopo madarakani Bw. Yusuf Manji kuhusu kufanyia marekebisho Katiba yao halafu  wafanye uchaguzi  hadi sasa mambo hayo mawili hayajafanyiwa kazi.

“Kwa mujibu wa  sheria Yanga haina Uongozi wa Kikatiba wala Kisheria ambao kwa hali iliyopo sasa ungeweza kuteua Kamati ya Uchaguzi,  Kama Kifungu F Ibara ya 45 cha Katiba ya Yanga kinavyoeleza, alisema Kiganja”.

Aliendelea kuwa,  kwa mujibu wa Sheria ya BMT Na. 12 ya mwaka 1967 na   marekebisho yake Na. 6 ya mwaka 1971 pamoja na Kanuni za Baraza na   Kanuni za Msajili namba 442 za mwaka 1999.  Baraza linaiagiza TFF kufanya  haya.

“Uchaguzi wa Yanga ufanyike na mchakato wake uanza wiki hii na kutaka  Uongozi mpya wa Yanga kuwepo madarakani katika muda usiozidi tarehe 30 Juni, 2016, Baraza kazi zetu ni pamoja na kuhakikisha hatuvunji Katiba za Wadau wetu, alieleza Kiganja.

Hata hivyo ameagiza  katika uchaguzi huo itumike Katiba ya mwaka 2010 huku     akiwataka   Watakaoingia madarakani kuingiza vipengele vya mabadiliko ndani ya Katiba ya Yanga kama ambavyo Mdau wao Mkuu TFF atakavyowalekeza.

“Kadi za Wanachama wa Yanga katika Uchaguzi huo zitumike zile zilizowahi kutumika katika Chaguzi zilizopita, zenye saini ya Mwenyekiti na Katibu wa Yanga na sio Kadi za CRDB au za Benki ya Posta, alisema na kuongeza.

“Nawaagiza TFF kuanza Mikutano ya kuweka taratibu za Uchaguzi kuanza ndani ya wiki hii na wasimamie Uchaguzi huo, alisema Katibu Mkuu”.

Aliendelea  kuwa,  TFF wahakikisha Vilabu vyote vinavyoshiriki Ligi Kuu kufanya Uchaguzi, akiondoa Klabu ya Simba, Cost Union na African Sports ambavyo tayari wamefanya chaguzi zao na Vilabu vilivyobaki visisitizwe vifanye Uchaguzi mara moja.

“Kanuni za TFF kuweka Sheria kali zinazotekelezeka ili kudhibiti ujanja ujanja wa baadhi ya Vilabu kukwepa kufanya Uchaguzi, “alisisitiza Kiganga”.

Kaimu Katibu Mkuu alisisitiza kuwa anavitaka Vyama na Mashirikisho ya Michezo nchini ambayo hayajafanya Uchaguzi, kufanye Uchaguzi ili Vilabu, Vyama na Mashirikisho hayo yatawaliwe Kisheria.

Mwisho.

49 total views, 1 views today

Fuatilia Mchezo, like:
0

Leave a Reply

Michezo ni yetu wote, fuatilia, Wataarifu wengi

Follow by Email14
Facebook
Facebook
YouTube0
YouTube
Google+0
Google+
http://nationalsportscouncil.go.tz/blog/2016/04/19/bmt-yaiagiza-tff-kuhakikisha-klabu-ya-yanga-inafanya-uchaguzi/">
RSS