Mashindano ya Chess kuanza 23 April Mwaka huu.

Na Mwandishi wetu-BMT

Mashindano ya mchezo wa chess  ya mtu mmoja mmoja ya ukanda wa Afrika 4.2 yajulikanayo kama (2016 Africa Zone 4.2 Individual Chess Championship) yanatarajiwa kuanza  tarehe 23 mpaka  30 April mwaka huu  hapa jijini Dar es salaam.

pix 1
Mwenyekiti wa Chama cha mchezo wa Chess Tanzania (TCA) Bw. Geofrey Mwanyika akiongea na waandishi wa Habari hawapo pichani kuhusu mashindano ya mtu mmoja mmoja ya ukanda wa Afrika 4.2 yajulikanayo kama (2016 Africa Zone 4.2 Individual Chess Championship). Yatakayofanyika hivi karibuni Jijini Dar es salaam.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Akizungumza hayo mbele ya waandishi wa habari Mwenyekiti wa chama cha mchezo huo nchini (TCA) Bw. Geofrey Mwanyika amesema kuwa michuano hiyo itafanyika katika Hoteli ya Peacock jijini Dar es salaam Tanzania ikiwa mwenyeji wa mashindano hayo.

Aidha Bw. Mwanyika ameinisha nchi ambazo zimethibitisha washiriki wake ni Uganda, Kenya, Rwanda, Burundi, Djibout, Eritrea,Somalia,Ethiopia, Sudan Kusini na wenyeji Tanzania

“Jumla ya washiriki 32 watachuana katika mashindano hayo ambayo yamegawanyika katika makundi mawili ya Wanaume na Wanawake na kati ya nchi hizo ambazo zinashiriki Sudan na Seychells hazijathibitisha kushiriki”. Aliongeza Bw. Mwanyika.

pix 2
Katibu wa Chama cha Mchezo wa Chess Tanzania (TCA) Bw. Nurdin Hassuji ambaye pia ni Bingwa wa Taifa wa mchezo huo akiongea na waandishi wa Habari hawapo pichani kuhusu mashindano ya mtu mmoja mmoja ya ukanda wa Afrika 4.2 yajulikanayo kama (2016 Africa Zone 4.2 Individual Chess Championship), kulia ni Mwenyekiti wa Chama hicho Bw. Geofrey Mwanyika.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Kwa upande wa Katibu wa TCA  Bw. Nurdin Hassuji ambaye pia ni Bingwa wa Taifa wa mchezo huo amesema kuwa zawadi za washindi ni Dola 4500  za Kimarekani ambazo zitagawanywa kwa watakaoshinda.

Aidha Bw. Hassuji amewataka wadau wa Michezo  na waandishi wa habari kujitokeza siku hiyo ili kuipa sapoti timu yao na kuutangaza mchezo ujulikane na kupendwa zaidi nchini.

Mbali  na hayo Bw. Hassuji amesema kuwa mchezo huo wameupa kipaumbele na kwenda kuufundisha mashuleni kwa sababu inawasaidia wanafunzi kuweza kufikiri kwa haraka zaidi na kufanya mwanafunzi awe mwepesi kwenye kupambanua mambo.

 

24 total views, 1 views today

Fuatilia Mchezo, like:
0

Leave a Reply

Michezo ni yetu wote, fuatilia, Wataarifu wengi

Follow by Email14
Facebook
Facebook
YouTube0
YouTube
Google+0
Google+
http://nationalsportscouncil.go.tz/blog/2016/04/20/mashindano-ya-chess-kuanza-23-april-mwaka-huu/">
RSS