CHAMIJATA NA SHIMBATA WARIDHIA KUUNDWA KWA CHOMBO KIMOJA KITAKACHOSIMAMIA VYAMA VYA MICHEZO YA JADI.

Chama cha michezo ya jadi Tanzania (CHAMIJATA) pamoja na Shirikisho la mchezo wa bao Tanzania (SHIMBATA) wameridhia maelekezo kutoka Baraza la Michezo la Taifa (BMT) yanayowataka kuunda chombo kimoja kitakachosimamia michezo ya jadi Tanzania.

KGANJA1
Kaimu Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Bw. Mohamed Kiganja akieleza jambo kwa Wajumbe wa Michezo ya Jadi wakati wa kikao nao cha kujadili namna ya kuunda chombo kimoja ndani ya michezo ya jadi tarehe 22 Aprili mwaka huu.

Akizungumza katika mkutano nao mwishoni mwa wiki, Kaimu Katibu Mkuu wa Baraza Bw. Mohamed Kiganga alisema, nia ya Baraza ni kuona michezo ya Jadi inakuwa na inaiwakilisha nchi vizuri katika mashindano mbalimbali.
“Inawezekana hatuitendei au tunaitendea haki michezo ya jadi, alisema Kiganja”.
Alieleza kuwa, kumekuwa na mgawanyiko mkubwa katika michezo ya jadi ndiyo maana ameamua kukutane na viongozi, wanachama na wadau wa michezo huo ili kuweka utaratibu utakaoleta maendeleo kwani michezo ya jadi haitatoka kwa utaratibu uliopo sasa hivi, alisema”.
“ Ni imani yangu tukiitumia michezo hii vizuri, Tanzania itatangazwa na kupata sapoti ya watu kutoka sehemu tofauti kwakuwa michezo ni ghali na nina vyama zaidi ya 48 Serikali haiwezi kumudu kusaidia michezo yote , alieleza Kiganja”.
Aliongeza kuwa kazi ya Serikali ni kusajili ambao ni msaada mkubwa wa kukifanya chama kisaidiwe, vilevile kuweka mazingira mazuri ya Vyama kutawalika kama kuwa na katiba ya chama.
Rai yangu kwenu ni kuwa na chombo kimoja kitachoendesha michezo ya Jadi pamoja na vyombo vingine vinavyosimamia michezo mbalimbali vitakavyowajibika kwa chombo kimoja, alisisitiza Kiganja”.
“Nimewaita niwauzie wazo langu tulijadili kwa pamoja”.
Kwa upande wake Mwenyekiti na muasisi wa CHAMIJATA Mohamed Kazingumbe alisema, niko mbele kuvisaidia vikundi vya michezo mbalimbali tuwe na Shirikisho la michezo ya jadi lenye kufuata sheria na taratibu zote.
Naye Rais wa SHIMBATA Bw. Monday Likwepa alisema, tunaunga mkono kwa kuwa ni jambo la maendeleo na ni chombo kitakacholeta heshima na kushauri iundwe kamati kama TOC.
Wajumbe wote walikubaliana ambapo iliundwa Kamati kuu itakayoshughulika na katiba ya chombo kimoja pamoja na kamati ndogo ndogo zitazoshughulika na katiba za mchezo mmoja mmoja na kuwajibika kwa kamati kuu.
Kamati kuu iliundwa na Wakuu wa vyama vyote viwili Monday Likwepa (SHIMBATA), Mohamed Kazingumbe (CHAMIJATA), pamoja na mtu mmoja mmoja kutoka kila mchezo Rajabu Lulanga- kulenga shabaha, Sofia Kimega- kukuna Nazi, Ishengoma Mwombeki-kuvuta kamba, Anitha – Mdako, Amina Said- kusuka ukili, Goodluck Swai- Mieleka, Ester Samwel Bao huku mchezo wa Kirumbizi ukikosa mwakilishi.
Majukumu ya kamati hiyo ikiwa ni kupendekeza jina la Shirikisho, kuratibu kazi za kamati ndogo ndogo, kuandaa katiba, kuhamasisha kamati ndogo kutekeleza majukumu yao ikiwemo katiba za mchezo husika na kushirikisha Baraza, Wanasheria na wataalamu wa michezo katika kuundaa katiba zao huku wakitakiwa kuwasilisha Baraza utekelezaji wao wa kwanza baada ya wiki mbili.

KGANJA4
Picha ya pamoja ya kamati kuu ya Wajumbe wa michezo ya Jadi baada ya kikao

189 total views, 1 views today

Fuatilia Mchezo, like:
0

Leave a Reply

Michezo ni yetu wote, fuatilia, Wataarifu wengi

Follow by Email14
Facebook
Facebook
YouTube0
YouTube
Google+0
Google+
http://nationalsportscouncil.go.tz/blog/2016/04/22/chamijata-na-shimbata-waridhia-kuundwa-kwa-chombo-kimoja-kitakachosimamia-vyama-vya-michezo-ya-jadi/">
RSS