TANZANIA MWENYEJI WA MASHINDANO YA RIADHA CHINI YA MIAKA 20 YA AFRIKA MASHARIKI NA KATI (EAAR)

Tanzania ni mwenyeji wa mashindano ya riadha ya Vijana chini ya Miaka 20 ya Afrika Mashariki na Kati (EAAR), ambayo yanatarajiwa kufanyika Aprili 29 hadi 30 katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Kaimu Katibu Mkuu wa Shirikisho la Riadha Tanzania (RT), Ombeni Zavalla, alisema kwamba wapenzi wa riadha ambao wapo mbali na Dar es Salaam watafaidika kuona mashindano hayo kupitia Azam televisheni kwa kuwa inatarajia kuonyeshwa moja kwa moja ‘live.
Aliongeza kuwa, mashindano hayo yanatarajiwa kushirikisha nchi 11 Tanzania Bara ambaye ni mwenyeji wa mashindano, Somalia, Djibouti, Kenya, Uganda, Rwanda, Sudan, Ethiopia, Eritrea na Zanzibar.
Alisema mwisho wa nchi kuthibitisha ilikuwa juzi usiku na timu zote tayari zimethibitisha isipokuwa Sudan Kusini.
“Kwa sababu muda umekwisha na hatujapata uthibitisho kutoka Sudan Kusini wala taarifa zozote basi itakuwa imejitoa kwenye mashindano hayo hivyo zimebaki nchi kumi,” alisema.
Aliendelea kwamba wao kama waandaaji, tayari wamekamilisha kila kitu na timu ya Tanzania Bara iko kambini ikiendelea kujifua.
“Timu imeingia kambini wiki iliyopita katika hosteli za Filbert Bayi huko Kibaha, Pwani, ikiwa na jumla ya wachezaji 27 ambao wana afya nzuri na wapo tayari kwa mashindano hayo,” alisema

29 total views, 1 views today

Fuatilia Mchezo, like:
0

Leave a Reply

Michezo ni yetu wote, fuatilia, Wataarifu wengi

Follow by Email14
Facebook
Facebook
YouTube0
YouTube
Google+0
Google+
http://nationalsportscouncil.go.tz/blog/2016/04/25/tanzania-mwenyeji-wa-mashindano-ya-riadha-chini-ya-miaka-19-ya-afrika-mashariki-na-kati-eaar/">
RSS