PROF. ELISANTE OLE GABRIEL AFUNGUA RASMI MICHUANO YA RIADHA YA UMRI CHINI YA MIAKA 20

Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel amefungua rasmi mashindano ya Riadha ya nchi za Afrika Mashariki na Kati ya umri chini ya miaka 20 yaliyoanza leo katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

Katika ufunguzi huo Prof. Elisante alieleza kuwa vijana hawana budi kujituma ipasavyo na kuonyesha vipaji vyao kwakuwa michezo ni ajira na imewanufaisha wengi.

Rais wa Shirikisho la Riadha Kenya Jenerali mstaafu Jackson Tuwei(aliyesimama) akizungumza kabla hajamkaribisha Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaana Michezo Prof.Elisante OleGabriel.(aliyevaa miwani amekaa),Bw. Tuwei alisisitiza kufanya michezo ya mara kwa mara ili kujenga umoja na mshikamano katika eneo la Afrika Mashariki

“Rai yangu kwenu ni kuhakikisha mnaimarisha uhusiano wenu vizuri kupitia michezo hii ili kuendeleza nchi zetu”. Alisema Prof. Elisante.

Prof Elisante aliongeza kuwa, anatoa ombi kwa wadau mbalimbali kuunga mkono shughuli za riadha kwani ni mchezo rahisi kuwekeza.

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu ambaye pia ni Rais wa Shirikisho la RiadhaTanzania (RT)Bw.Anthony Mtaka akizungumza jambo wakati wa ufunguzi rasmi wa mashindano ya 10 ya ‘Eastern junior championship’ katika riadha yanayofanyika katika uwanja waTaifa jijini Dar es Salaam tarehe 29-30 April 2016.Wengine pichani ni Katibu Mkuu wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Prof.Elisante Ole Gabriel(wa pili kulia),Rais wa shirikisho la Riadha kenya Generali mstaafu Jackson Tuwei (watatu kulia) na Dk.Eng Siddig Ibrahim kutoka Sudan.

Mashindano hayo yanatarajiwa kufanyika kwa siku mbili kuanzia leo tarehe 29 hadi 30 Aprili na yanashirikisha nchi kumi zikiwemo Kenya, Uganda, Rwanda, Djibouti, Ethiopia, Somalia, Sudan, Zanzibar, Sudani kusini, na mwenyeji Tanzania.

ELISANTE3
Timu ya washiriki kutoka Tanzania wakipita mbele ya mgeni rasmi Katibu Mkuu wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof Elisante Ole Gabriel (hayupo pichani) kabla ya ufunguzi kuanza wa mashindano ya Riadha ya 10 ya East Africa Junior Championship yanayofanyika uwanja wa Taifa Dar es salaam.

20 total views, 1 views today

Fuatilia Mchezo, like:
0

Leave a Reply

Michezo ni yetu wote, fuatilia, Wataarifu wengi

Follow by Email14
Facebook
Facebook
YouTube0
YouTube
Google+0
Google+
http://nationalsportscouncil.go.tz/blog/2016/04/29/prof-elisante-ole-gabriel-afungua-rasmi-michuano-ya-riadha-ya-umri-chini-ya-miaka-20/">
RSS