HASSUJI AJINYAKULIA CHEO KATIKA MASHINDANO YA CHESS YA UKANDA WA 4.2

chess3

Mtanzania Nurdin Hassuji amefanikiwa kujinyakulia cheo cha ‘Candidate Master’ katika mashindano ya Chess ya ukanda wa 4.2 yalifanyika kuanzia tarehe 22 hadi 30 Aprili mwaka huu katika ukumbi wa Peacock Hotel, jijini Dar es Salaam.

Hassuji amefanikiwa kupata cheo hicho baada ya kumfunga Joseph Maigua wa Kenya kwa pointi 4.5 kati ya 9 ambapo awali cheo hicho kilishikiliwa na mchezaji mmoja tu wa Tanzania Bw. Yusuf Mdoe katika mashindano yaliyofanyika mjini Kampala, Uganda mwaka jana.

Mashindano hayo yalijumuisha nchi 12 ambazo ni Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, South Sudan, Sudan, Eritrea, Djibouti, Somalia, Egypt, Ethiopia na wenyeji Tanzania huku yakivunja rekodi ya kuwa na ushiriki wa nchi nyingi.

Mchezaji wa Misri Fide Master Kandhil Adham amefanikiwa kuwa mshindi wa mashindao hayo baada ya kuenda suluhu katika raundi ya mwisho na mchezaji kutoka Burundi Ezra Paul Chambers na kujinyakulia pointi 7 wakati raia mwenzake Fide Master Sobh Amrou akiwa mshindi wa pili na wote kufanikiwa kupata cheo cha ‘International Master’.

Mshindi wa tatu ni Fide Master Harold Wanyama wa Uganda aliyeshinda kwa pointi 6 na kujinyakulia cheo cha ‘International Master Norm’ huku jumla ya wachezaji 13 upandewa wanaume wakijipatia vyeo na wawili katika kundi la wanawake.

Wachezaji wengine wa Tanzania ni mwenye cheo Candidate Master Yusuf Mdoe, ambaye amemaliza kwa pointi 4.5 na Mwenyekiti wa Chama cha Chess Tanzania Eng. Geoffrey Mwanyika aliyejinyakulia pointi 4 pamoja na Hemed Mlawa.

'Candidate master' Mchezaji na Katibu wa chama cha mchezo Tanzania Nurdin Hassuji.
‘Candidate master’ Mchezaji na Katibu wa chama cha mchezo Tanzania Nurdin Hassuji.

Kwa upande wa wanawake Anawa Martha Fredy wa Tanzania’s amemaliza mashindano kwa pointi moja na Mmisri Woman Grandmaster Wafa Shrook akiwa mshindi wa mashindano haya baada ya kujinyakulia pointi 9.

Refari Vinay Choudary amefanikiwa kupata International Arbiter Norm, na Refarii msaidizi Lyasenga John and Sunday Manara wamefanikiwa kupata Fide Arbiter Norm.

Mwenyekiti wa Chama cha Chess Tanzania Eng. Geoffrey Mwanyika amesema kwamba chama chake kinaandaa mkakati wa kuchagua Team ya Taifa itakayowakilisha Tanzania katika mashindano ya 42nd Chess Olympiad mjini Baku, Azerbaijan kuanzia tarehe 1 hadi 14 Septemba 2016.

Aliongeza kuwa, wanapanga kuiwakilisha Tanzania kwa upande wa wanaume na wanawake, wakati Kamati ya maadalizi ya 42nd Chess Olympiad ikimpatia mwaliko mwamuzi pekee Tanzania FA Vinay Choudary kuwa mmoja wa waamuzi katika mashindano hayo.

Mashindano hayo yalifunguliwa na Rais wa Africa Chess Confederation Bw. Lewis Ncube wa Zambia na Rais wa Ukanda wa Chess wa 4.2 Bw. Vianney Luggya kutoka Uganda huku wakikipongea Chama Cha Chess Tanzania kuandaa mashindano hayo kwa kiwango cha juu sana.

22 total views, 1 views today

Fuatilia Mchezo, like:
0

Leave a Reply

Michezo ni yetu wote, fuatilia, Wataarifu wengi

Follow by Email14
Facebook
Facebook
YouTube0
YouTube
Google+0
Google+
http://nationalsportscouncil.go.tz/blog/2016/04/30/hassuji-ajinyakulia-cheo-katika-mashindano-ya-chess-ya-ukanda-wa-4-2/">
RSS