MHESHIMIWA ANASTANZIA WAMBURA AFUNGA MASHINDANO YA RIADHA YA UMRI CHINI YA MIAKA 20.

Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastanzia Wambura amefunga michuano ya Riadha ya nchi za Afrika Mashariki na Kati iliyofanyika katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

mheshiwaaa3

Mashindano hayo yalifanyika mwisho wa wiki kwa siku mbili yakishirikisha nchi 10 ambazo ni Djibouti, Ethiopia, Kenya, Rwanda, Somalia, Sundan, Uganda, Zanzibar, Sudan Kusini na wenyeji Tanzania Bara.

Katika mashindano hayo, Tanzania imefanikiwa kuongeza uzoefu wa mashindano ya dunia na mwaandaaji, na kushika nafasi ya sita baada ya kupata medali moja ya dhahabu, moja ya fedha na tano zikiwa za shaba.

mheshiwaaa1

Tanzania imechukua medali hiyo ya dhahabu kupitia mwanariadha Rose Seif kutoka shule Filbert Bay, aliyewashinda wakenya katika mbio ndefu.

Wakati Tanzania Bara ikishika nafasi hiyo, Kenya waling’ara, baada ya kushika nafasi ya kwanza kwa kujinyakulia medali 13 za dhahabu, fedha 8 na nne za shaba ikifuatiwa na Uganda iliyopata dhahabu 4,fedha 5 na shaba 3.

Nafasi ya tatu ilikwenda kwa Sudan walijinyakulia medali 3 za dhahabu , 2 za fedha na 2 za shaba huku Ethiopia ikishika nafasi ya nne kwa kupata medali 2 za dhahabu, 2fedha na 1 ya shaba.
Zanzibar wao wameshika nafasi ya tano ikiwa na dhahabu mbili, fedha mbili na shaba nne wakati nafasi ya saba ikishikiliwa na Rwanda iliyopata fedha moja na shaba moja.

Nafasi ya nane ikienda kwa Sudan Kusini na Djibouti baada ya kupata medali moja ya shaba kila mmoja na Somalia ilishika nafasi ya mwisho bila kupata medali yoyote.

mheshiwa2

203 total views, 1 views today

Fuatilia Mchezo, like:
0

Leave a Reply

Michezo ni yetu wote, fuatilia, Wataarifu wengi

Follow by EmailO
Facebook
Facebook
YouTube0
YouTube
Google+0
Google+
http://nationalsportscouncil.go.tz/blog/2016/05/01/mheshimiwa-anastanzia-wambura-afunga-mashindano-ya-riadha-ya-umri-chini-ya-miaka-20/">
RSS