BMT KUKUTANA NA VYAMA NA WADAU WA MICHEZO MWISHO WA WIKI.

Mtendaji Mkuu wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Bw. Mohamed Kiganja anatarajia kufanya mkutano na Vyama/Mashirikisho na Wadau wa michezo wa Mkoa wa Dar es salaam siku ya jumamosi tarehe 7 Mei mwaka huu katika Uwanja wa uhuru kuanzia saa 4:00 asubuhi hadi saa 7 mchana jijini Dar es salaam.

Akizungumza na Waandishi wa Habari kwa niaba ya Kaimu Katibu Mkuu , Afisa Habari wa Baraza Najaha Bakari alisema, lengo la mkutano huo ni kujadili maendeleo ya Michezo Mkoa wa Dar es salaam.

Hata hivyo, Mtendaji Mkuu wa BMT, Bw. Kiganja amemwomba Katibu wa Kamati ya Michezo Mkoa wa Dar es salaam ambaye ni Afisa Michezo wa Mkoa kuwapa taarifa hiyo Viongozi wa Vyama /Mashirikisho ya Michezo wa Mkoa , Wilaya, Wadau toka Taasisi mbalimbali wanaotumia michezo katika kazi zao kuhudhuria mkutano huo, “alisema Najaha”.

Aliongeza kuwa Baraza limejipanga kufanya kazi kwa karibu zaidi na wadau wake katika nchi nzima ili kuona michezo inaenda mbele ila tunaanza na Mkoa wa Dar es salaam.

Mtendaji Mkuu wa Baraza anatoa wito kwa wapenda maendeleo Mkoa wa Dar es salaam kujitokeza kwa wingi ili kwa pamoja tuweke mikakati ya maendeleo ya michezo ya Mkoa huo na nchi nzima kwa ujumla, “ alieleza Najaha”.

51 total views, 1 views today

Fuatilia Mchezo, like:
0

Leave a Reply

Michezo ni yetu wote, fuatilia, Wataarifu wengi

Follow by Email14
Facebook
Facebook
YouTube0
YouTube
Google+0
Google+
http://nationalsportscouncil.go.tz/blog/2016/05/04/bmt-kukutana-na-vyama-na-wadau-wa-michezo-mwisho-wa-wiki/">
RSS