KIGANJA: FUATENI SHERIA NA TARATIBU KATIKA KUENDESHA MICHEZO.

Mtendaji Mkuu wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Bw. Mohamed Kiganja amewataka Viongozi wa vyama vya michezo kufuata sheria na taratibu katika kuendesha michezo nchini.

Rai hiyo ameitoa katika mkutano na Viongozi wa vyama vya michezo Mkoa wa Dar es salaam, Wadau na Taasisi zinazoendesha kazi zao kupitia michezo uliofanyika mwisho wa wiki katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam.

kganja4

 

 

“Sheria ya Baraza la Michezo la Taifa (BMT) imeweka bayana taratibu za kuendesha michezo nchini kupitia ngazi mbalimbali na uwepo wa michezo na Maafisa michezo ni kwa mujibu wa sheria, alisisitiza Kiganja”.
Aliendelea kuwa, kuna vyama havifanyi chaguzi katika wakati husika na kuongoza kimakosa.
“Utawala bora ndani ya chama ndio utatufanya tuondoke hapa tulipo, uchaguzi ufanyike na tufuate demokrasia, alisema Kiganja”.
Kiganja aliuagiza Uongozi wa Mkoa wa Dar es salaam kuhakikisha vyama vya michezo vya Mkoa huo wanafanya uchaguzi, vyama ambavyo vitashindwa kufanya uchaguzi kulingana na katiba zao viongozi wake wafukuzwe na kuongeza kuwa.
“Afisa Michezo Mkoa wa Dar es salaam, itisha mkutano na viongozi wa mpira wa kikapu mpange taratibu za uchaguzi na hakikisha uchaguzi unafanyika, alieleza Mtendaji Mkuu wa Baraza”.
“Naagiza viongozi wa vyama vya michezo kutengeneza mipango kazi ya chama, kalenda ya matukio ya mwaka na kuwasilisha taarifa za utekelezaji katika ngazi husika, alisema”.
Hata hivyo, aliviagiza vyama kufikisha michezo mashuleni na kuwa na ligi za rika zote na kutambua kuwa vipaji huanzia ngazi ya shule.
Mtendaji Mkuu wa Baraza, Bw. Kiganja ameaviagiza vyama vya michezo Mkoa wa Dar es salaam kuanzisha michezo ajili ya Wazee na Wanawake ili kusimamia michezo kwa makundi hayo.
Kiganja alimtaka Afisa michezo Wilaya ya Temeke kusimamisha mchakato wa kuanzisha chama cha soka Wilaya ya Kigamboni hadi mchakato wa Serikali utakapokamilika.

Aliendelea kuwa Uongozi wa Mkoa wa Dar es salaam uhakikisha Wilaya zake zote zinakuwa na Maafisa Michezo wenye sifa za michezo na kuwataka Maafisa Michezo wa Mkoa kukaa na wadau jogging ili kuanzisha na kuchagua vyama vya Wilaya.

kganja2

Awali Mgeni Rasmi, Katibu Tawala wa Mkoa aliyewakilisha na Afisa Elimu wa Mkoa wa Dar es salaam Bw. Raymond Mapunda, alisema kuwa, vyama vya michezo vinakaribishwa mashuleni kwa kufuata taratibu na kuwa na Walimu wa michezo husika.

Kiganja alieleza kuwa, Mkoa wa Dar es salaam ndiyo kioo, tukifanikiwa sisi Taifa zima litafanikiwa na tunadhamana kubwa, na kuongeza kuwa ataenda Mikoa yote na kukutana na wadau ili kuhakikisha kunaondoka tulipo.

kganja3

127 total views, 1 views today

Fuatilia Mchezo, like:
0

Leave a Reply

Michezo ni yetu wote, fuatilia, Wataarifu wengi

Follow by Email14
Facebook
Facebook
YouTube0
YouTube
Google+0
Google+
http://nationalsportscouncil.go.tz/blog/2016/05/10/kiganja-fuateni-sheria-na-taratibu-katika-kuendesha-michezo/">
RSS