BMT LIMEPOKEA MAPENDEKEZO YA RASIMU NA JINA LA CHOMBO KIMOJA CHA KUSISMAMIA MICHEZO YA JADI NCHINI.

Baraza la Michezo la Taifa (BMT) limepokea mapendekezo ya jina na rasimu ya kwanza ya Katiba ya chombo kimoja kitakachosimamia michezo ya jadi kutoka kwa Kamati kuu iliyoundwa tarehe 22 Aprili na kuagizwa kufanya hayo baada ya wiki mbili.

DSC06756

Agizo hilo lilitolewa na Kaimu Katibu Mkuuwa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Bw. Mohamed Kiganja  katika Mkutano wake na  chama cha michezo ya jadi Tanzania (CHAMIJATA) na Shirikisho la mchezo wa bao Tanzania (SHIMBATA) kilichofanyika  tarehe 22 Aprili mwaka huu katika Ukumbi wa uwanja wa uhuru jijini Dar es salaam.

Katika kikao hicho Mtendaji Mkuu wa Baraza  aliagiza Taasisi hizo mbili kuvunjwa na kuundwa chombo kimoja cha kusimamia michezo ya jadi ambapo kila mchezo ulitakiwa  kujitegemea na kuwajibika  kwa chombo kimoja.

Akiwasilisha hayo kwa Waandishi leo asuhuhi kabla ya kupokea Rasimu hiyo kwa niaba ya Mtendaji Mkuu wa BMT, Afisa Maendeleo ya Michezo na mlezi ya michezo ya jadi nchini Bw. Milinde Mahona alieleza kuwa, katika mkutano huo Wajumbe wote waliafiki wazo la Mtendaji Mkuu wa Baraza.

DSC06763
Rasimu ya kwanza na mapendekezo ya jina la chombo Kimoja kitakachosimamia michezo ya jadi nchini.  

Mahona alisema, baada ya makubaliana hayo ya wadau wote wa mchezo wa jadi iliundwa Kamati maalum ya watu 10 ambao  walitokana na Mjumbe mmoja kutoka kila mchezo wa jadi na  Viongozi wakuu wa Taasisi hizo huku wakitakiwa baada ya wiki mbili kuwasilisha rasimu ya Katiba na pendekezo la jina la chombo hicho na kila Wadau wa mchezo husika walielekezwa kuandaa katiba yao  wakiratibiwa na Kamati kuu.

“Wanachofanya leo ni maelekezo yaliyotokana na kikao hicho na wameenda na muda, alieleza Mahona”.

Kamati kuu ya chombo kimoja iliwakilishwa na;

  1. Mohamed Kazingumbe – CHAMIJATA
  2. Mandey Likwepa – SHIMBATA
  3. Rajabu Lulanga – Mdau mchezo wa kulenga shabaha
  4. Esta Samwel – Mdau mchezo wa Bao
  5. Amina Saidi Mwangia – Mdau mchezo wa kusuka ukili
  6. Ali Saidi Tunku – Mdau mchezo wa kirumbizi/Fimbo
  7. Ishengoma Mwombeki – Mdau mtu mwenye ulemavu mchezo wa kuvuta kamba
  8. Anita Anas Ali – Mdau mchezo wa mdako
  9. Gooluck Swai – Mdau mchezo wa mieleka ya jadi
  10. Sofia Kinega – Mdau wa mchezo kusuna nazi

 

Aidha,  Baraza la Michezo la Taifa (BMT) linaiagiza Kamati kuu kuhakikisha ifikapo mwishoni mwa mwezi wa sita mwaka huu Katiba zote za kusimamia michezo ya jadi nchini kikiwema chombo kikuu na vyombo vidogo vya kila mchezo kukamilika na ieleweke kuwa michezo ya jadi ni muhimu  kwa maendeleo ya Taifa kwani ipo kwa jamii na ni rahisi kuchezwa katika mazingira yao, alisema Mahona”.

 

 

DSC06758
Wadau wa michezo ya jadi waliohudhuria katika tukio la kukabidhi rasimu ya kwanza ya Katiba ya chombo kikuu cha kusimamia michezo ya jadi leo jijini Dar es salaam.

 

 

21 total views, 1 views today

Fuatilia Mchezo, like:
0

Leave a Reply

Michezo ni yetu wote, fuatilia, Wataarifu wengi

Follow by Email14
Facebook
Facebook
YouTube0
YouTube
Google+0
Google+
http://nationalsportscouncil.go.tz/blog/2016/05/12/bmt-limepokea-mapendekezo-ya-rasimu-na-jina-la-chombo-kimoja-cha-kusismamia-michezo-ya-jadi-nchini/">
RSS