IBUENI AKINA BAYI, IKANGAA NA SAMSON WENGINE.

Serikali imesema inapenda kuona Jeshi linarudisha enzi zake  za kuibua vipaji na kuandaa wanamichezo wenye uwezo wa kufanya vizuri katika mashindano ya kitaifa na kimataifa na kuiletea sifa nchi kama ilivyokuwa zama za wachezaji mahiri akiwemo Filbert Bayi, Juma Ikangaa na Samson Ramadhan.

NAPE 1
1. Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akihutubia wakati wa kufungua mashindano ya tatu ya kombe la Mkuu wa Majeshi (CDF Cup – 2016)kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Hayo yameelezwa leo na Waziri wa habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye wakati akifungua muhula wa tatu wa mashindano ya Kombe la Mkuu wa Majeshi (CDF CUP- 2016) uliofanyika kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam.

NAPE3

 

 

 

 

 

 

Mashindano hayo yameanza rasmi leo na yanatarajiwa kuhitimishwa tarehe 6 Juni mwaka huu.

Waziri Nape alisema, changamoto iliyopo kwa Timu zetu za Taifa hivi sasa ni kupata matokeo mabaya zinaposhiriki katika mashindano ya kimataifa na kushindwa kuiletea nchi ushindi na medali mbalimbali kama ilivyokuwa zamani.

“Sote tunafahamu kuwa miaka ya nyuma timu za majeshi ndizo zilizotoa uwakilishi bora katika mashindano kitaifa na kimataifa, hivyo kiu ya wapenda michezo wengi mimi nikiwa mmojawapo kuona enzi hizo za Jeshi kuwa kituo bora katika michezo zinarudi  sasa, “alisema Waziri Nape na kuongeza kuwa;

“Ni ukweli usiopingika kuwa nchi nyingi zilizopiga hatua katika maendeleo ya michezo ni matokeo ya kuwekeza katika programu za kuibua, kukuza na kuendeleza vipaji, naomba  kulipongeza JWTZ kwa jitihada zake za dhati katika kupitia program yake ya “Twalipo Youth Sports Foundation”.

Waziri Nape ametoa wito kwa watu binafsi, taasisi na mashirika nchini kutumia teknolojia ya kisasa kuanzisha na kuendeleza programu za kuibua na kukuza vipaji katika michezo pamoja na kuwaendeleza wanamichezo kielimu kwakuwa michezo na Elimu vinaenda sambamba.

NAPE5

38 total views, 1 views today

Fuatilia Mchezo, like:
0

Leave a Reply

Michezo ni yetu wote, fuatilia, Wataarifu wengi

Follow by Email14
Facebook
Facebook
YouTube0
YouTube
Google+0
Google+
http://nationalsportscouncil.go.tz/blog/2016/05/24/ibueni-akina-bayi-ikangaa-na-samson-wengine/">
RSS