GIDABUDAY: RIADHA NDIO MWANZO WA  MICHEZO YOTE.

MEI 26,2016

Mratibu wa mashindano ya mbio za watoto 2016 Bw. Gidabuday kutoka RT amesema riadha ndio mwanzo wa michezo yote.

Amezungumza hayo leo wakati wa mkutano na  Waandishi wa habari kuhusu mbio hizo uliofanyika katika ukumbi wa BMT jijini Dar es salaam.

“Washiriki ni watoto wa umri kuanzia miaka 2 na nusu hadi 16 kwa wasichana na wavulana ambapo mbio zitaanzia 50m, 100m, 1km, 2km, na 5km, alisema Gidabuday”.

Alieleza kuwa, Benki ya Azania imedhamini  mashindano hayo ya  riadha kwa watoto  yajulikanyo kama ‘ Azania Bank Kids Run 2016’ yanayotarajia kufanyika Juni 5, mwaka huu katika viwanja vya mnazi mmoja jijini Dar es Salaam.

 Afisa Masoko wa Benki ya Azania, Othman Jibrea (mwenye tai) akifafanua jambo kwa waandishi hawapo pichani wakati wa mkutano na waandishi jijini Dar es salaam, Afisa habari wa BMT Najaha Bakari (kushoto), Mjumbe wa Kamati ya Ufundi wa Shirikisho la Riadha Tanzania (RT) Tulo Chambo (wapili kulia) Mratibu wa mashindano ya Azania Bank Kids Run 2016’  Bw. Gidabuday (kulia).
Afisa Masoko wa Benki ya Azania, Othman Jibrea (mwenye tai) akifafanua jambo kwa waandishi hawapo pichani wakati wa mkutano na waandishi jijini Dar es salaam, Afisa habari wa BMT Najaha Bakari (kushoto), Mjumbe wa Kamati ya Ufundi wa Shirikisho la Riadha Tanzania (RT) Tulo Chambo (wapili kulia) Mratibu wa mashindano ya Azania Bank Kids Run 2016’ Bw. Gidabuday (kulia).

Kwa upande wake Afisa Masoko wa Benki hiyo, Othman Jibrea, alisema wanatarajia kutumia zaidi ya  milion 130 kwa ajili ya  program hiyo.

Alisema lengo la kufanya hivyo ni kurudisha faida waliyoipata kutoka kwa jamii  kuinua michezo ambapo program hiyo itakuwa ni endelevu.

“Baada ya kufanya kazi kwa muda mrefu na jamii tumeamua kudhamini mchezo wa riadha ikiwa ni  katika kuangali jinsi ya kukuza vipaji vya watoto hivyo  katika mashindano haya tunatarajia kutumia zaidi ya milioni 130 katika  kurudisha faida  tuliyoipata,” alisema.

Kwa upande wake Mjumbe wa Kamati ya Ufundi wa Shirikisho la Riadha Tanzania (RT), Tulo Chambo alisema kuwa wameshukuru benki hiyo kujitokeza kudhamini mashindano  hayo kwa watoto ambayo itasaidia kutoa hamasa zaidi katika mchezo huo.

Alisema kumekuwa na changamoto kubwa hasa ya udhamini kwenye michezo hivyo   wanaomba  mashirika na taasisi nyingine kujitokeza  kudhamini michezo kama ilivyofanya benki hiyo.

“Hawa watoto hawataishia hapa ila tunataka kuwatengeneza na kuwajenga kwenye ushindani wa riadha, tunawashukuru Azania Benki na tunaomba wengine wajitokeze ili kufanikisha maendeleo ya  mchezo wa riadha nchini,” alisema Chambo.

Alifafanua kuwa katika mashindano hayo zitakuwepo zawadi mbalimbali zitakazotolewa kwa washindi wa mbio tofauti na washiriki kwa ujumla.

MWISHO.

206 total views, 1 views today

Fuatilia Mchezo, like:
0

Leave a Reply

Michezo ni yetu wote, fuatilia, Wataarifu wengi

Follow by Email5
Facebook
Facebook
YouTube0
YouTube
Google+0
Google+
http://nationalsportscouncil.go.tz/blog/2016/05/26/gidabuday-riadha-ndio-mwanzo-wa-michezo-yote/">
RSS