WATU WENYE ULEMAVU WATAKIWA KUENDELEZA MICHEZO.

Mei 26

Balozi Mdogo wa Marekani nchini, Virginia Blaser amewataka washiriki wa mafunzo ya michezo kwa watu wenye ulemavu kuwa  chachu ya kuendeleza michezo kwa kundi hilo.

Blaser ameyasema hayo leo wakati akifungua mafunzo ya siku 4 yatakayohitimishwa kwa bonanza la michezo kwa watu wenye ulemavu lilifanyika katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

mafunzo5

“ Serikali ya Marekani inafanya kazi kwa karibu sana na Kamati ya Paralimpiki ya Tanzania na ina historia ya kuwa na program za kubadilishana uzoefu kama ilivyo hii, hivyo washiriki wa mafunzo haya mnatakiwa mkafanyie kazi ambacho mmefundishwa ili kuendeleza michezo kwa watu wenye ulemavu, alisema Bleser”.

Aliendelea kuwa, kufanya kazi kwa pamoja kunaweza kujenga jamii bora ambapo watu wote bila kujali ulemavu wao au kutokuwa walemavu wanaweza kushiriki katika michezo na kunufaika katika nchi zao.

Mafunzo hayo yanaendeshwa na Wataalamu kutoka chuo kikuu cha Kentucky cha Marekani,  na  Kamati ya michezo ya Tanzania (Tanzania Paralympic Commitee) na kushirikisha watu wenye ulemavu kutoka Tanzania na Kenya.

mafunzo2

Mafunzo hayo yamefadhiliwa na Serikali ya Marekani kupitia Wizara ya mambo ya nje na yanajumuisha wakufunzi na makocha kutoka Chuo kikuu cha Kentacky Marekani, Uingereza, Canada na Kenya ambao wanatoa mafunzo ya michezo mbalimbali ya Watu wenye ulemavu ikiwemo riadha, miruko, mitupo, wavu, kikapu na soka.

Mafunzo hayo ni mwendelezo wa programu ya michezo kwa watu wenye ulemavu kwa waliopata mafunzo itakayodumu kwa muda wa mwaka mmoja na nusu kwa ufadhili wa Serikali ya Marekani.

mafunzo4

 

19 total views, 1 views today

Fuatilia Mchezo, like:
0

Leave a Reply

Michezo ni yetu wote, fuatilia, Wataarifu wengi

Follow by Email14
Facebook
Facebook
YouTube0
YouTube
Google+0
Google+
http://nationalsportscouncil.go.tz/blog/2016/05/26/watu-wenye-ulemavu-watakiwa-kuendeleza-michezo/">
RSS