SERIKALI YATAKA UFAFANUZI KUTOKA PST.

27 Mei, 2016

Serikali imelitaka Shirikisho la ngumi la PST kutoa ufafanuzi  kuhusu kuchezesha watoto katika mapambano ya ngumi ya utangulizi.

Hayo yamesema jana na Kaimu Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Bw. Mohamed Kiganja alipozungumza na Waandishi wa habari jijini Dar es salaam.

Kiganja alieleza kuwa,  amemuandikia barua Mkurugenzi wa Pugilistic Syndicate of Tanzania (PST), Emanuel Mlundwa na kumpa siku saba (7) kutoa maelezo ya kina kabla Serikali haijachukua hatua zaidi.

Hivi karibuni PST iliandaa mapambano ya ngumi jijini Dar es salaam huku katika baadhi ya mapambano hayo ya utangulizi yalishirikisha watoto wadogo wa umri tofauti tofauti.

Mtendaji Mkuu wa BMT alisema, Sheria ya Tanzania hairuhusu watoto kupambanishwa kwani kunaweza kuwasababishia matatizo katika vichwa vyao.

Alisema kuwa, watu wengi wanafanya makosa kuoanisha sheria za nchi yetu na nchi zingine.

“Kwani sheria zetu haziruhusu kabisa kupambanisha watoto”

Aliongeza kuwa, tena watoto hao walipambanisha ulingoni katika usiku mkubwa kitu ambacho nacho si sahihi kwakuwa watoto hawatakiwi katika kumbi za burudani mida hiyo.

 

13 total views, 1 views today

Fuatilia Mchezo, like:
0

Leave a Reply

Michezo ni yetu wote, fuatilia, Wataarifu wengi

Follow by Email14
Facebook
Facebook
YouTube0
YouTube
Google+0
Google+
http://nationalsportscouncil.go.tz/blog/2016/05/27/serikali-yataka-ufafanuzi-kutoka-pst/">
RSS