UCHAGUZI KLABU YA YANGA UPO KAMA SERIKALI ILIVYOELEJKEZA.

31 Mei 2016

Serikali imesema uchaguzi wa klabu ya Yanga utafanyika kama ilivyoelekeza.

Hayo yameelezwa leo na Mtendaji Mkuu wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Mohamed Kiganja alipofanya kikao na Waandishi wa habari Ofisini kwake jijini Dar es salaam.

Kiganja ameeleza kuwa, wanaongeza muda wa kuchukua na kurudisha fomu za uchaguzi kwa siku tano hivyo wagombea waendelee kuchukua hadi kufikia jumapili tarehe 5 Juni mwaka huu.

“Uchukuaji wa fomu ulishaanza na mwisho ilikuwa leo lakini wapo watu na wengine wamo ndani ya TFF na wengine nje ambao wanafanya michakato ya kukwamisha kufanyika kwa uchaguzi huo, alisema Kiganja na kuongeza kuwa;

Serikali haina nia mbaya na klabu hiyo bali kuona vilabu, vyama na mashirikisho ya michezo wanaheshimu sheria, kanuni na katiba zilizopo.

“Hayo yanayofanyika kuelekea uchaguzi siyo utashi wa mtu, bali kutekeleza katiba ya Yanga, hivyo vikao mbalimbali vinavyafanyika vya wanachama au wadau vilenge kufanikisha uchaguzi badala ya kuvuruga zoezi hilo”, alisema.

Kiganja alieleza kuwa, hawazitambui kadi mpya za uanachama za klabu hiyo, bali wanazitambua kadi za zamani ambazo ndizo zitakazotumika katika uchaguzi huo.

“Tafsiri ya kadi ni mali ya klabu lakini unapokuwa na kadi ya benki maana yake ni mali ya benki hiyo na sijui kama mwenyekiti wa klabu atakuwa na mamlaka nayo”, alieleza Kiganja.

“Mwanachama yoyote akalipie kadi yake ya zamani mwaka mmoja aingie kwenye uchaguzi”, alisema.

Hivyo, sidhani kama ni halali kadi za benki kutumika katika uchaguzi kwa sababu, hazina saini ya mwenyekiti wa klabu wala ya kiongozi yoyote, tofauti na kadi za zamani ambazo zina saini za viongozi.

 

39 total views, 1 views today

Fuatilia Mchezo, like:
0

Leave a Reply

Michezo ni yetu wote, fuatilia, Wataarifu wengi

Follow by Email14
Facebook
Facebook
YouTube0
YouTube
Google+0
Google+
http://nationalsportscouncil.go.tz/blog/2016/05/31/uchaguzi-klabu-ya-yanga-upo-kama-serikali-ilivyoelejkeza/">
RSS