MASHINDANO YA RIADHA TAIFA KUFANYIKA JUNE 11.

 

Mashindano ya riadha ya Taifa yanatarajiwa kufanyika kwa siku moja tarehe 11 June badala ya tarehe 3 hadi 4 pamoja na tarehe 22 – 23 June kama ilivyoelezwa awali.

Akieleza hayo leo alipotembelea Ofisi za BMT Katibu Mkuu Msaidizi wa RT Ombeni Zavala amesema kuwa, wamebadili na kuwa tarehe hiyo kutokana na Uwanja wa Taifa ambao ungetumika katika mashindano hayo kuwepo kwa mechi ya kimataifa kati ya Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) na Timu ya Misri itakayofanyika tarehe 4 mwezi huu.

riadha-664x383
2. Wanariadha wakiwa katika mashindano katika moja ya mashindano

“Tarehe hiyo tumeipanga na kuafikiana katika kikao cha kamati ya utendaji ya RT tulichokaa jana tarehe 1 June mwaka huu”, alisema na kuongeza kuwa;

“Tumewaelekeza kila Mkoa kulete wanariadha watano (5) wenye viwango badala ya idadi ambayo tuliwaeleza mwanzo”

Zavala alieleza kuwa, watakaofuzu katika mashindano hayo wataendelea na maandalizi kwa ajili ya kufuzu mashindano ya Oliympiki ya mwaka huu Brazili ili kuongeza idadi wa wanariadha watatu waliopo Kilimanjaro wakiendelea kujifua ambao wamefuzu michuano hiyo.

Hata hivyo, kwakuwa kiwanja chetu hakipo kwenye viwango vya Oliympiki watakaofuzu watashiriki mashindano ya Afrika yatakayofanyika Durban kuanzia tarehe 21 hadi 26 June na Kenya 28-29 mwezi huu ili kufuzu viwango vya Olimpiki, alisema Zavala.

Aidha, Zavala anayaomba Makampuni, Mashirika na Watu binafsi kujitokeza kuendelea kuwasaidia ili wafanikishe mashindano hayo kwakuwa bado maandalizi hayajakamilika.

44 total views, 1 views today

Fuatilia Mchezo, like:
0

Leave a Reply

Michezo ni yetu wote, fuatilia, Wataarifu wengi

Follow by Email14
Facebook
Facebook
YouTube0
YouTube
Google+0
Google+
http://nationalsportscouncil.go.tz/blog/2016/06/02/3178/">
RSS