MHESHIMIWA ANASTAZIA WAMBURA MGENI RASMI AZANIA KIDS RUN 2016.

Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Anastazia Wambura anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika  Mbio za Watoto za Azania Kids Run 2016,  zitakazofanyika Viwanja vya Mnazi Mmoja Jumapili Juni 5 jijini Dar es Salaam.

wambura

Akizungumza jijini Dar es Salaam leo, Mratibu wa Azania Kids Run 2016, zinazodhaminiwa na Benki ya Azania, Wilhelm Gidabuday, amesema kuwa Naibu Waziri Wambura anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika kinyang’anyiro hicho kitakachokuwa na mbio za kategori tano.

Gidabuday amebainisha kuwa, maandalizi yote ya Azania Kids Run 2016 yanaenda vema, ikiwamo idadi kubwa ya wazazi na walezi kujitokeza kusajili watoto wao, huku akiwataka wengi kutumia siku mbili zilizobaki kuhakikisha wanawapa vijana wao nafasi ya kushiriki.

azania 3
Mwanafunzi Rachel Stephen wa Shule ya Sekondari ya Mburahati (kulia) na Ali Muhidin kutoka Shule ya Msingi Muungano wakizungumzia ushiriki wao katika mbio hizo.

“Wazazi ndio waamuzi wa ushiriki wa watoto, tunawashauri wazazi wawape nafasi kushiriki katika mbio hizo”, alisema Gidabuday.

“Mbio hizi zinazotarajia kushirikisha zaidi ya watoto 2,000, zinatarajia kufanyika Jumapili Juni 5, 2016 kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja, zikihusisha watoto chini ya miaka 16, alisema Gidabuday.

Amewasisitiza wazazi, walezi na wadau kujitokeza kusajili watoto wao na kwamba fomu bado zinapatikana katika matawi yote ya Benki ya Azania, Ofisi za Baraza la Michezo la Taifa (BMT) zilizoko Samora Avenue na Ofisi za Shirikisho la Riadha Tanzania (RT).

Gidabuday ametumia nafasi hiyo kuwahakikishia wazazi na walezi wa watoto watakaoshiriki Azania Kids Run 2016 kuwa, usalama wa watoto wao wakati wa shindano utakuwa kipaumbele chao na kuwatoa hofu ya usalama wakati wa kukimbia.

“Barabara zote zitakazotumiwa na watoto kukimbilia zitakuwa na uangalizi maalum ikiwa ni pamoja na gari za huduma ya kwanza na matibabu kwa watakaohitaji kupatiwa huduma hizo,” amesema Gidabuday katika mkutano na wanahabari Dar es Salaam.

Ofisa Masoko Mwandamizi wa Azania Bank, Othman Jibrea, amezitaja zawadi za washindi mbalimbali wa mbio hizo, huku akiweka msisitizo kwa kutawaka wazazi kuendelea kusajili watoto wao kuwa sehemu ya tukio hilo la kihistoria.

“Mshindi wa kwanza mbio za Kilomita 5 ni Sh. 200,000, mshindi wa pili Sh. 150,000 na mshindi wa tatu sh. 100,000, pamoja na medali, begi lenye vifaa vya shule na sare za michezo, wakati mshindi wa nne hadi wa 10 watapata kifuta jasho cha sh. 15,000,” amesema.

Katika mbio za kilomita 2, Jibrea alitaja zawadi kuwa ni sh. 100,000 kwa mshindi, huku atakayeshika nafasi ya pili akitarajiwa kulamba sh. 75,000 na wa tatu kujitwalia sh. 50,000, kategori ambayo pia washindi wa nne hadi wa 10 watapata kifuta jasho cha sh. 15,000.

Aidha, amebanisha kuwa, kategori ya mbio za kilomita moja mshindi atatwaa sh. 75,000, huku wa pili akibeba sh. 50,000 na wa tatu akijishindia sh. 40,000, ambako pia washindi wa nne hadi wa 10 watapata kifuta jasho kama kilivyotajwa hapo juu.

Pia kutakuwa na mbio za mita 50 na 100, ambazo zitakimbiwa na watoto chini ya miaka mitatu, ambapo washindi wote watafunguliwa akaunti katika Benki ya Azania, itakayokuwa na kianzio cha sh.15,000, sanjari na begi la shule lenye vifaa vyote muhimu.

 

 

 

72 total views, 1 views today

Fuatilia Mchezo, like:
0

Leave a Reply

Michezo ni yetu wote, fuatilia, Wataarifu wengi

Follow by Email14
Facebook
Facebook
YouTube0
YouTube
Google+0
Google+
http://nationalsportscouncil.go.tz/blog/2016/06/03/mheshimiwa-anastazia-wambura-mgeni-rasmi-azania-kids-run-2016/">
RSS