SAMATA AKABIDHIWA EKERI TANO KUWEKEZA KATIKA MICHEZO.

Mchezaji wa Tanzania anayechezee timu ya KRC Genk ya nchini Belgium Mbwana Samata amekabidhiwa ekari tano (5) na Mtandano wa Wasanii Tanzania (SHIWATA) kwa ajili ya kuwekeze katika michezo kwa kujenga kituo cha michezo Mkoani Pwani Wilaya ya Mkuranga.

SAMATA2

Hayo yamefanyika kutokana na juhudi mchezaji huyo anazoonesha katika mchezo na kuiletea nchi sifa kimataifa, hivyo SHIWATA kuona ni bora kumwezesha eneo hilo ili ajenge kituo cha michezo kwa maendeleo ya watoto wanamichezo wa Tanzania.

Eneo hilo amekabidhiwa na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Sanaa Leah Kihimbi kwa niaba ya Waziri wa Habari ,Utamaduni , Sanaa na Michezo Mheshimiwa Nape Nnauye, eneo lililopo katika kijiji cha Wasanii Mwanzega Kata ya Mbezi Wilaya ya Mkuranga.

Kihimbi alieleza kuwa, uamuzi waliochukua Mtandao wa Wasanii Tanzania (SHIWATA) niwakuigwa na wengi kwakuwa atakapowekeza Samata utafaidisha wanamichezo vijana Wakitanzania ambao watajiajiri na kuitangaza nchi mbali kama afanyavyo Samata.

“Sanaa na michezo ni ajira na pia ni biashara na ndio maana Samata anatafutwa kununuliwa na mataifa mengi”, alisema Kihimbi.

Kwa upande wake Baba yake Mzazi Mbwana Mzee Ally Samata Kwa niaba yake, alisema kuwa , kituo hicho kitakuwa ni mfano na kitawanufaisha na kuwavuta wengi kutoka hapa nchini na hadi nje ya Tanzania.

Hata hivyo, Mwenyekiti wa Mtandao wa wasanii Kassim Twalibu ameiomba Serikali kuwawekea miundombinu ikiwemo, barabara, maji na umeme ili kukiinua kijiji hicho na iwe rahisi kwa uwekezaji huu kwa Samata na wanachama wengine

 

46 total views, 1 views today

Fuatilia Mchezo, like:
0

Leave a Reply

Michezo ni yetu wote, fuatilia, Wataarifu wengi

Follow by Email14
Facebook
Facebook
YouTube0
YouTube
Google+0
Google+
http://nationalsportscouncil.go.tz/blog/2016/06/06/samata-akabidhiwa-ekeri-tano-kuwekeza-katika-michezo/">
RSS