TAASISI ZINAZOENDESHA NGUMI ZA KULIPWA NCHINI ZATAKIWA KUFUATA SHERIA NA KUWATENDA HAKI MABONDIA.

Taasisi na Mapromota wanaoendesha ngumi za kulipwa wametakiwa kufuata sheria zilizowekwa katika kuendesha mchezo huo pamoja na kuwatendea haki Mabondia nchini.

Hayo yamesemwa leo na Kaimu Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Bw. Mohamed Kiganja alipokutana na baadhi ya Mabondia wa kulipwa na Mapromota ili kuwaeleza kuhusu kufuata sheria na kuwatendea haki Mabondia wa mchezo huo.

Kiganja alieleza kuwa, mtandao wa ngumi za kulipwa umekuwa na ufisadi sana kutokana na baadhi ya Mapromota kutotenda haki kwa Mabondia kufuatia mapambano mbalimbali wanayoshiriki kitaifa na kimataifa.
“Baadae mabondia mnaishia kuilaumu Serikali kwamba haiwatendei haki huku ni Mapromoto kutoweka wazi haki zenu wakati wa mapambano,”alisema Kiganja na kuongeza kuwa:

“Hakuna Serikali inayotaka kugandamiza watu wake lazima tuwaeleze sheria inasemaje na zipi haki zenu”.

“Kwanini mnawanyanyasa sana hawa watoto, msiwadhulumu haki zao, mkidhulumiwa niambieni mimi niko pamoja na nyie,”alisisitiza Kiganja.
Hata hivyo, amezitaka taasisi zinazoendesha ngumi za kulipwa kuelewa kuwa Taasisi inayofahamika na Serikali na ambayo imesajiliwa kwa kuwa na leseni ya BMT ni TPBC pekee, hivyo wanatakiwa kupitia huko kabla ya BMT.

“Endesheni michezo yenu kwa kuitambua TPBC ndiyo chama pekee tunachokitambua,”alisema.

“Kama taasisi inataka Serilikali iitambue hata kama imesajiliwa sehemu ingine lazima ije BMT kukata leseni kwakuwa ndio chombo pekee kinachosimamia michezo nchini.”

Awali Raisi wa TPBC Chaurembo Palaso alieleza kuwa, TPBC watashirikiana na Baraza la Michezo la Taifa (BMT) ili kuhakikisha Sheria za mchezo huo zinafuatwa na haki za Mabondia zinaonekana.

Kikao hicho kiliwashirikisha baadhi Mabondia wa kulipwa, Mapromota, Makocha na Mabondia wa zamani.

31 total views, 1 views today

Fuatilia Mchezo, like:
0

Leave a Reply

Michezo ni yetu wote, fuatilia, Wataarifu wengi

Follow by Email14
Facebook
Facebook
YouTube0
YouTube
Google+0
Google+
http://nationalsportscouncil.go.tz/blog/2016/08/04/taasisi-zinazoendesha-ngumi-za-kulipwa-nchini-zatakiwa-kufuata-sheria-na-kuwatenda-haki-mabondia/">
RSS