MAFUNZO YA MAKOCHA WANAWAKE YAFUNGULIWA RASMI

Mafunzo ya siku tano ya Walimu Wanawake wa mpira wa miguu nchini iliyoandaliwa na Shirikisho la mpira wa miguu duniani FIFA kwa kushirikiana na TFF imefunguliwa rasmi leo na Mjumbe wa  BMT Bi Jenipher Mmasi katika ukumbi wa  TFF Ilala jijini Dar es Salaam.
Mafunzo hayo yanaanza kutolewa leo tarehe 5 hadi 9 mwezi huu na mkufunzi toka FIFA Bi Andrea Ronebaugh ikihusisha walimu 26 toka mikoa mbali mbali nchini yenye lengo la kuinua soka la Wanawake nchini.

jeniffer1
Mgeni rasmi Bi. Jennifer Mmasi (kulia) akitoa neno la shukrani kwa Mkufunzi wa kozi hiyo Bi Andrea Rodebaugh (kushoto) kuja kwa ajili ya kozi hiyo.

Mmasi ameishukuru FIFA kuona umuhimu wa kuleta Mkufunzi nchini kwetu na hasa kwa ajili ya Makocha Wanawake.

Hata hivyo, amewataka Makocha hao kuitumia nafasi hiyo adhimu vizuri na  kutoa elimu watakayopata kwa Wanawake wengine badala ya kuvihifadhi vyeti na kukalia ujuzi.

“Tumieni fursa hakuna kitakachoshindikana, ukiamua kichwani kuwa unaweza Mwalimu anafuata,”alisisitiza Mmasi.

Kozi hiyo inakuja siku chache kabla ya kuanza kwa ligi ya Taifa ya soka kwa Wanawake ambayo inatarajiwa kuanza kutimua vumbi mwezi ujao.

jennifer3
Bi. Jennifer Mmasi (katikati) akisema jambo na Makocha watakaofaidika na mafunzo hayo (hawapo pichani), Mkufunzi wa kozi hiyo Bi Andrea Rodebaugh (kushoto) na Mwenyekiti wa soka la Wanawake nchini Amina Ngaluma (kulia).

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa soka la Wanawake nchini Amina Ngaluma amewataka makocha hao wakimaliza kozi wasikae nyumbani bali watumie ujuzi huo kuendeleza wanawake wenzao ili kuiweka nchi kwenye ramani kwa soka la kinamama.

“Mi niwakumbushe mkimaliza kozi hii mkirudi nyumbani tumieni elimu mliyoipata kwa ajili ya maendeleo ya soka la Wanawake na hiyo ndiyo dhamira ya FIFA,” alisema Ngaluma.

Katika hatua nyingine,  Mkufunzi wa kozi hiyo Bi Andrea aliwapongeza TFF kuomba kuandaa mafunzo hayo ili kuwapata makocha wengi Wanawake ambao watakuwa chachu ya kuinua soka kwa kinamama.

76 total views, 2 views today

Fuatilia Mchezo, like:
0

Leave a Reply

Michezo ni yetu wote, fuatilia, Wataarifu wengi

Follow by Email14
Facebook
Facebook
YouTube0
YouTube
Google+0
Google+
http://nationalsportscouncil.go.tz/blog/2016/09/06/mafunzo-ya-makocha-wanawake-yafunguliwa-rasmi/">
RSS