PAN AFRICAN YAAHIDI KURUDI KATIKA UBORA WAKE WA AWALI

Klabu ya mpira wa miguu ya Pan African imeahidi kurudi katika ubora wake wa awali katika soka la Tanzania.

Hayo yameelezwa leo na Katibu Mkuu wa klabu hiyo, Bw.Saddy Mateo katika mkutano wao na Waandishi wa Habari uliofanyika katika ukumbi wa Baraza la michezo la Taifa (BMT) jijini Dar es salaam.

Mateo ameeleza kuwa, kufuatia mgogoro wa Wanachama wa klabu hiyo uliodumu kwa muda mrefu kuanzia mwaka 2007, Serikali imesaidia kupitia ngazi tofauti za usuluhishi ambapo Wanachama wameondoa tofauti zao na kuhakikisha  inaanza kufanya kazi kwa weledi mkubwa ili kurudisha hadhi iliyopoteza kwa muda.

“Ni kweli tumepoteza muda mwingi  katika migogoro ila tunawaahidi Wanachama, Wadau na Mashabiki waendelee kutupa moyo na nguvu za kuirudisha Pan African katika ushindi wake wa ligi kuu na kuiondoka katika daraja la pili la Mkoa,” alisema Mateo.

Aliendelea kuwa, wameandaa Mkutano Mkuu utakaofanyika siku ya jumapili tarehe 11 mwezi huu kuanzia saa  nne asubuhi katika Uwanja wa Taifa na kuongeza kuwa:

Wanachama  wa zamani waliorudi watatakiwa kujaza fomu na kulipia ada zao za nyuma  kabla ya kuingia katika mkutano huo, huku Wanachama wapya wakiidhinishwa  siku hiyo na kutakiwa kuendelea kujitokeza kujiandikisha kwa wingi.

Fomu za uanachama zinaanza kutolewa na kulipiwa kuanzia leo Septemba 8 hadi siku hiyo ya Mkutano Mkuu.

Hata hivyo, katika kurejesha mtizamo chanya wa klabu hiyo mkutano huo pia utazungumzia  mpango wa uchaguzi ulioahirishwa hapo awali.

Mkutano huo uliwahusisha Makamu Mwenyekiti Bw. Ally Hemed Ally, Katibu Mkuu Msaidizi  Mohamed Hashimu Mkweche, Mjumbe Carlos Mwinyimkuu, Baraza la Wazee alikuwepo Seifu Malinda wakiongozwa na Katibu Mkuu Saddy Mateo.

53 total views, 1 views today

Fuatilia Mchezo, like:
0

Leave a Reply

Michezo ni yetu wote, fuatilia, Wataarifu wengi

Follow by Email14
Facebook
Facebook
YouTube0
YouTube
Google+0
Google+
http://nationalsportscouncil.go.tz/blog/2016/09/09/3264/">
RSS