KIGANJA: CHAMA KILICHOSAJILIWA KISIFANYE KAZI NA CHAMA KISICHOSAJILIWA

Septemba  09, 2016

Kaimu Katibu Mkuu wa Baraza la Taifa (BMT) Bw. Mohamed Kiganja amevitaka vyama vya ngumi za kulipwa vilivyosajili kutofanya kazi na vyama ambavyo havijasajiliwa.

Hayo ameyasema jana alipofanya kikao na Viongozi  wa Chama cha ngumi za kulipwa cha TPBC ambacho  kipo kisheria kwa kupita ngazi zote za usajili  na kupewa  dhamana ya kusimamia ngumi za kulipwa nchini.

Katibu Mkuu huyo  ameleza kwamba, Chama chochote kinachotaka kufanya kazi ya michezo lazima kipitia ngazi zote zinazotakiwa kisheria ili kufanya kazi ya mchezo husika nchini, yaani kipate usajili wa jina la kampuni la biashara kutoka BRELLA,  kisajiliwe na mamlaka ya mapato (TRA)ili kilipe kodi kulingana na kazi inazofanya  lakini pia lazima usajili ufanyike katika Wizara husika inayosimamia michezo.

“Nafanya kazi na nyie TPBC kwa kuwa  mnafuata sheria na mmepita  sehemu zote hizo,  tusaidiane ili mchezo huu uchezwe kwa kufuata  taratibu  ” alisema Kiganja.

Pia alieza kuwa, Chama kikiwa na matatizo kianze kuyazungumzia ndani ya chama, na endapo hakitafikia muafaka kuna taratibu za kufuata  kwa kupitia ngazi tofauti na siyo kukimbilia mahakamani, alisema Kiganja.

Hata hivyo,  Bw. Kiganja amewaagiza Viongozi wa chama cha ngumi za kulipwa Tanzania (TPBC) kuifanyia marekebisho na maboresho Katiba yao kwa kuwashirikisha wadau wao iendane ya yale  aliyoagiza na kukubaliana katika kikao hicho na  kuiwasilisha kwake baada ya wiki mbili.

Vilevile amewataka Viongozi wa mchezo huu kuacha kuwa Mawakala na Mapromota  bali waongoze na kutumia  elimu na ujuzi wao pekee ili kuhakikisha haki inatendeka katika mapambano  mbalimbali.

Aliendea kuwa, hawana budi kufanya kazi kwa kufuata sheria na Katiba yao vitakavyowafanya  wafuate taratibu  na kuondokana na mfumo wa kizamani.

Katika hatua nyingine Bw. Kiganja amewataka TPBC kuona umuhimu wa kuwa na Afisa habari wao ili kila mtu asiwe msemaji wa chama, wawe na Afisa Masoko na Mtunza  kumbukumbuku  ili  chama kiwe na siri na  taarifa zao kutunza kitaalamu.

Kwa upande wake Rais wa TPBC Bw. Chaurembo  kwa niaba ya Chama hicho alisema kuwa, wanapata faraja kupata kiongozi anayetaka ngumi hizo ziendeshwe kwa kufuata sheria na kuwafaidisha mabondia ambapo, aliahidi  kuyafanyia kazi maelekezo ya Mtendaji Mkuu huyo wa BMT.

Kikao hicho kilichoitishwa na Kaimu Katibu Mkuu wa BMT Bw. Mohamed Kiganja,  kilihudhuriwa na Afisa anayeshughulikia ngumi za kulipwa Apansia Lema, Afisa Habari Najaha  Bakari na  viongozi mbalimbali wa TPBC wakiongozwa na  Rais Bw. Chaurembo Palaso, Katibu Mkuu Chatta Michael, Makamu wa Rais Lituka Dusso, Promota Sadick Kinyogori, Kamati ya Sheria Yahya Poli, Kocha Ally Matimbwa, na Kamati ya Ufundi Ally Bakari na Mweka hazina wao Joe Ane.

103 total views, 1 views today

Fuatilia Mchezo, like:
0

Leave a Reply

Michezo ni yetu wote, fuatilia, Wataarifu wengi

Follow by Email14
Facebook
Facebook
YouTube0
YouTube
Google+0
Google+
http://nationalsportscouncil.go.tz/blog/2016/09/09/kiganja-chama-kilichosajiliwa-kisifanye-kazi-na-chama-kisichosajiliwa/">
RSS