WUSHU TAIFA KUFANYIKA MWISHO WA WIKI.

Mashindano ya 3 ya Taifa ya Mchezo wa Wushu ‘Kung Fu’ yanatarajiwa kufanyika kwa siku mbili mwisho wa wiki hii kuanzia tarehe 17 hadi 18 katika uwanja wa ndani wa Taifa jijini Dar es salaam.
Akizungumzia mashindano hayo leo wakati wa mkutano na vyombo vya habari katika ukumbi wa Ofisi za tamaduni za china (Chinese culture), Rais wa mchezo wa Wushu Tanzania Bw,Mwarami Shaweji Mitete alieleza kuwa mashindano hayo yatashirikisha Mikoa 8 ya Tanzania ukiwemo mwenyeji Dar es salaam, Pwani, Morogoro, Tanga, Mtwara, Lindi, Mbeya na Pemba.
 
Aliendelea kuwa, timu 31 zinatarajiwa kuchuana ndani ya shindano hilo kutoka ndani ya wanachama wa Chama cha Wushu Tanzania (TWA) na waalikwa kutoka vyama tofauti vya sanaa za mapigano.
 
“Tunatarajia mashindano kufunguliwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda na kufungwa na Waziri mwenye dhamana ya Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye”, alisema Mitete na kuongeza kuwa:
 
Lengo la mashindano hayo ni kupata timu bora ya Taifa itayoiwakilisha nchi katika mashindano ya kimataifa pamoja na kujenga uhusiano mzuri ndani ya wanachama wa (TWA) na wananchi.
 
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa TWA Bw.Salehe Mtaula alieleza kuwa, zawadi mbalimbali zatatolewa kwa washindi ikiwemo, Vikombe, Medali, Fedha taslimu na zawadi zingine kama feni, simu na cheti.
 

36 total views, 1 views today

Fuatilia Mchezo, like:
0

Leave a Reply

Michezo ni yetu wote, fuatilia, Wataarifu wengi

Follow by Email14
Facebook
Facebook
YouTube0
YouTube
Google+0
Google+
http://nationalsportscouncil.go.tz/blog/2016/09/14/wushu-taifa-kufanyika-mwisho-wa-wiki/">
RSS