SHERIA IFUATWE KUHAKIKISHA VYANZO VYA MAPATO VYA BARAZA VINAWASILISHWA

19 Octoba, 2016.

Sheria ya Baraza la Michezo la Taifa Na.2 ya mwaka 1967 na marekebisho yake Na. 6 ya mwaka 1971 lazima itekelezwe kuhakikisha vyanzo vya mapato vyote vya BMT vinawasilisha ili kusaidia maendeleo ya michezo nchini.

Hayo yameelezwa leo na Mwenyekiti wa Baraza la michezo la Taifa Bw. Dioniz Malinzi wakati wa kikao chake na  Kamati ya utendaji  ya baraza  kilichofanyika tarehe 19 Octoba mwezi huu katika ukumbi wa uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

“Kamati ya fedha, utafiti  na mipango  kwa kushirikiana na Mhasibu hakikisheni mnafuatilia vyanzo vyote vya mapato ya Baraza vya  kisheria ili tuweze kufanya maendeleo ya michezo kupitia vyanzo hivyo,”alisisitiza  Malinzi.

Aliongeza  kuwa,  vilevile katika kuitekeleza sheria hiyo, viongozi wa vyama/mashirikisho na vilabu mbalimbali vya michezo nchini hawatakiwi  kugombea nafasi  zaidi ya mbili za uongozi  katika mchezo mmoja  kama sheria inavyoelekeza.

“Katibu Mkuu  andika  barua kwa vyama na vilabu vya michezo yote kuelekeza hilo, na waeleze waisome Sheria ya BMT  waielewe vizuri ili wasiende  kinyume nayo,”alieleza Malinzi.

Vile vile,  Kamati hiyo imeagiza kiongozi  yeyote wa chama anapotaka kujiuzulu lazima afuate Katiba ya chama na taratibu zingine za kisheria na siyo kujiuzulu kwa kutumia vyombo vya habari bila kufuata taratibu za kikatiba kama alivyofanya kiongozi wa TAHA.

“Kamati ya nidhamu angalieni katiba ya chama hiki inasemaje kuhusu kujiuzulu kwa mwenyekiti wa TAHA,”alisema Mwenyekiti Malinzi.

Kamati tendaji  imesisitiza vyama na wadau wa michezo kuitekeleza na kuiheshimu sheria ya Baraza la michezo la Taifa (BMT) na kuacha kujiamulia wenyewe bali waelewe kuwa  sheria haibadilishi kwa maneno ila kwa sheria.

 

 

17 total views, 2 views today

Fuatilia Mchezo, like:
0

Leave a Reply

Michezo ni yetu wote, fuatilia, Wataarifu wengi

Follow by Email14
Facebook
Facebook
YouTube0
YouTube
Google+0
Google+
http://nationalsportscouncil.go.tz/blog/2016/10/19/sheria-ifuatwe-kuhakikisha-vyanzo-vya-mapato-vya-baraza-vinawasilishwa/">
RSS