SPUTANZA YAISHAURI TFF KUWEKA KANUNI

CHAMA cha wachezaji wa mpira wa miguu Tanzania (Sputanza) kimeshauri Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kuweka kanuni katika ligi itakayowataka wachezaji wote kuwa wanachama wa chama hicho ili kuepukana na migogoro ya mikataba inayowakuta.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Mwenyekiti wa Sputanza, Mussa Kissoky alisema wachezaji wengi hawana muda wa kusoma mikataba na kuielewa na kumtafuta mmoja kumwelekeza inakuwa ngumu.

Alisema njia nyepesi ya kuwapa elimu ni kuhakikisha wachezaji wote wa Ligi Kuu, Ligi Daraja la Kwanza wanajiunga na kuwa wanachama, hivyo kuwa rahisi kuelimishwa kuhusu masuala mbalimbali yanayowahusu.

“Matatizo mengi yanayowakumba wachezaji ni suala la mikataba, wengi hawana  muda wa kuisoma, wanachojua ni kusaini bila kujua utamfaidishaje,” alisema.

Kissoky alieleza kuwa,  kuna umuhimu wa kuweka  kanuni itakayowataka wachezaji kutumia wakala wanaotambuliwa na Sputanza na TFF katika masuala ya uhamisho na usajili wa wachezaji.

Aliongeza kuwa,  siku za usoni wanatarajia kurusha kipindi kwenye televisheni kuwaelimisha wadau wote wa mpira wa miguu masuala mbalimbali yanayohusu soka.

SPUTANZA imesajiliwa kwa lengo la kusaidia na kusimamia maslahi na mustakabali wa wachezaji wa soka Tanzania, kuboresha  uendeshaji ligi, vilabu na vyama vya soka ili kuleta tija ambayo wachezaji wangepaswa kuipata kupitia tasnia hii.

Vilevile kulifanya soka kuwa ni fursa ya ajira kwa wanachama wetu, fursa ambayo ikiratibiwa vizuri ki-ueledi na kwa uwazi itazalisha mtiririko mpana zaidi hususani katika pato la Taifa, jamii na mtu mmoja mmoja

SPUTANZA  ni chama cha wachezaji kama ilivyo kwa vyama vya wachezaji wa soka kwa nchi zingine ikiwemo, FUB – Footballers  Union of Botswana, PFA – Professional Footballers  Association – Uingereza, MLSPU – Major League  Soccer  Players  Union – Marekani na vingine.

 

111 total views, 1 views today

Fuatilia Mchezo, like:
0

Leave a Reply

Michezo ni yetu wote, fuatilia, Wataarifu wengi

Follow by Email5
Facebook
Facebook
YouTube0
YouTube
Google+0
Google+
http://nationalsportscouncil.go.tz/blog/2016/11/16/sputanza-yaishauri-tff-kuweka-kanuni/">
RSS