ZOEZI LA KUCHUKUA NA KURUDISHA FOMU ZA UCHAGUZI KWA RT LAKAMILIKA.

Zoezi la kuchukua na kurudisha fomu za uchaguzi kwa Chama cha Riadha Tanzania zilizokuwa zikitolewa katika  Ofisi za BMT, tovuti ya Baraza na Ofisi za RT, lililoanza tarehe 1 Novemba limemalizika jana tarehe 15 mwezi huu.

Rai hiyo ameitoa Afisa Michezo anayesimamia chama hicho Apansia Lema kwa wadau na waandishi waliotaka kujua mwisho wa  zoezi hilo, ambapo aliwaeleza kuwa umefikia mwisho kutokana na makubaliano kati ya RT na Baraza la michezo la Taifa.

“Zoezi hili limefungwa wagombea wajiandae na siku ya usaili na hatimaye uchaguzi,”alisema Lema.

Katika zoezi hilo, nafasi zote za uongozi zilizokuwa zinagombewa zimepata wagombea ambapo wengi wao wametetea nafasi zao za awali ikiwemo nafasi ya Rais ambayo Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony Mtaka anaitetea nafasi yake akiwa mgombea pekee.

Wakati nafasi ya Makamu wa Rais Utawala ina wagombewa wawili Mwenyekiti wa chama cha riadha Mkoa wa Dar es salaam Zainabu Mbiro na William Kallaghe akitetea nafasi ya awali, huku Makama wa Rais Ufundi ikiwa na mgombea mmoja anayetetea nafasi hiyo Dr. Hamad Ndee. Ambapo, nafasi ya Katibu  Mkuu ikiwa na wagombea 3 Michael Washa, Wilhelm Gidabuday na Gidamis Shahanga huku nafasi ya Katibu Mkuu msaidizi ikichukuliwa na Ombeni Zavalla akitetea nafasi yake.

Nafasi ya Mweka hazina ina mgombea mmoja Gabriel S. Liginyan huku nafasi ya ujumbe ikigombaniwa na wagombea 17 katika nafasi 10 zinazohitajika.

Uchaguzi wa  RT unatarajiwa kufanyika tarehe 27 Novemba huku usaili ukitarajiwa kufanyika tarehe 26 mwezi huu.

Wito wa Baraza kwa Mikoa ni kufanya chaguzi zao kabla ya siku ya uchaguzi wa Taifa wa RT na Mikoa ambayo haitafanya uchaguzi haitaruhusiwa kushiriki katika tukio hilo.

 

 

61 total views, 1 views today

Fuatilia Mchezo, like:
0

Leave a Reply

Michezo ni yetu wote, fuatilia, Wataarifu wengi

Follow by Email14
Facebook
Facebook
YouTube0
YouTube
Google+0
Google+
http://nationalsportscouncil.go.tz/blog/2016/11/16/zoezi-la-kuchukua-na-kurudisha-fomu-za-uchaguzi-kwa-rt-lakamilika/">
RSS