TIMU YA KABADDI YAREJEA NYUMBANI KUTOKA NCHINI INDIA

Novemba 21

Timu ya Kabbadi na ujumbe walioambatana nao  katika mashindano ya dunia yaliyofanyika kwa wiki mbili kuanzia tarehe 3-17 Novemba, 2016 imerejea mwisho wa wiki kutoka Mjini Punjab nchini China.

kganja
Mkuu wa Msafara Katibu mkuu wa Baraza la Michezo la Taifa Bw. Mohamedi Kiganja akiongea na waandishi kuhusu safari ya Punjab, katika mashindano hayo baada ya kutoka ndani ya Uwanja wa Nyerere jijini Dar-es-salaam.

Akizungumzia safari hiyo,  Mkuu wa msafara Katibu Mkuu wa BMT Bw. Mohamed Kiganja  ameeleza kuwa, walitegemea kurudi na ushindi lakini imekuwa tofauti kulingana na timu ambazo wamecheza nazo ni zenye uzoefu wa muda mrefu ukilinganisha na timu ya Tanzania mchezo ni mgeni kwao na mafunzo wamepata kwa muda mfupi.

“Tanzania ni mara ya kwanza kushiriki mashindano makubwa kama hayo huku mchezo ukiwa ni mgeni kwetu na timu imepata mafunzo kwa muda mfupi na kukutana na miamba yenye uzoefu wa miaka mingi katika mashindano ya mchezo huo,”alisema na kuongeza kuwa:

Hata hivyo pamoja na wachezaji kutofanya vizuri  tumeimarisha mahusiano kati ya mataifa haya mawili, ambapo wameahidi  kuendelea kutupa ushirikiano kwa  kuleta walimu wakufundisha mchezo huo  na imani yetu mashindano mengine timu ya Tanzania itafanya vizuri.

Kwa upande wake, kapteni wa timu ya Wanawake Salima Pontia  alisema kuwa, pamoja  na kutofanya vizuri  timu zetu tumejitahidi kutangaza utalii wa Tanzania ikiwemo Mlima Kilimanjaro, Mbuga za wanyama kama Serengeti na nyingine nyingi.

Kabaddi ni mchezo wenye asili ya mji wa Punjab nchini India ambapo mashindano hayo yalihusisha Mataifa mengi  ikiwemo USA , England, Spain, Denmark, Iran, Argentina, Canada, Kenya, Sweden, Australia, Tanzania, Sierra Leone, New Zealand, Mexico, na mwenyeji India.

49 total views, 1 views today

Fuatilia Mchezo, like:
0

Leave a Reply

Michezo ni yetu wote, fuatilia, Wataarifu wengi

Follow by Email14
Facebook
Facebook
YouTube0
YouTube
Google+0
Google+
http://nationalsportscouncil.go.tz/blog/2016/11/21/timu-ya-kabaddi-yarejea-nyumbani-kutoka-nchini-india/">
RSS