BMT LAFANIKIWA KUSIMAMIA UCHAGUZI WA RT KWA AMANI

Novemba 28,

Baraza la Michezo la Taifa limefanikiwa kusimamia uchaguzi wa Shirikisho la riadha Tanzania (RT) kufanyika kwa amani mwisho wa wiki Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

jamal-matokeo

Katika uchaguzi huo, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Anthony Mtaka amefanikiwa kutetea nafasi yake ya Urais akiwa mgombea pekee kwa kupata kura za ndiyo 73 na moja ya hapana kati ya kura 74 zilizopigwa.
mataka2
Huku Mwanaharakati mkubwa wa michezo wa riadha nchini, Wilhelm Gidabuday akiibuka mshindi wa nafasi Ukatibu Mkuu wa Riadha Tanzania (RT) katika uchaguzi huo.

Gidabuday ambaye anajulikana sana kwa kukosoa viongozi wa michezo huo katika vyombo vya habari, alishinda kiti hicho baada ya kupata kura 38 za ndiyo, huku Michael Washa akipata kura 24 na mwanariadha wa zamani, Gidamis Shahanga akiondoka na kura 11.

Gidabuday anachukua mikoba iliyoachwa wazi na Suleimana Nyambui ambaye hakugombea baada ya kuwa nchini Brunei akifundisha timu ya taifa ya riadha ya nchi hiyo.

 
makam
Makamu wa Kwanza wa Rais (Utawala), William Kalaghe aliibuka mshindi kwa kura 59 dhidi ya mpinzani wake Zainabu Mbiro aliyeondoka na kura 15 . Wakati makamu wa pili wa Rais (Ufundi), Dk Hamad Ndee alipata kura 70 za ndiyo na nne tu zilimkataa katika kinyang’anyiro hicho, ambacho hakuwa na mpinzani.

Katibu msaidizi ni Ombeni Zavalla aliyepata kura za ndiyo 70 huku tatu zikimkataa na moja ikiharibika wakati Mhazini ni Gabriel Liginyan aliyepata kura za ndiyo 67 na hapana 7.

Waliotwaa ujumbe wa Kamati ya Utendaji ni Lwiza John, Meta Petro, Robert Kalyahe, Dk Nassoro Matuzya, Rehema Killo, Zakaria Barie, Mwinga Mwanjala, Tullo Chambo, Christian Matembo na Yohana Misese.

Awali Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo la Taifa
kiganja

BMT, Mohamed Kiganja alisema kuwa RT ndio chama pekee cha michezo huo nchini kinachoongozwa na Mkuu wa Mkoa, “kwetu sisi (BMT) ni utajiri, hii ni dalili nzuri hivyo ukiboronga unapoteza nafasi zote mbili,” na kuongeza.

“Migogoro kwenye vyama inakimbiza wawekezaji na wafadhili, sio vyema pindi mambo ya ndani yanapokuwa hayaendi sawasawa kukimbilia kwenye vyombo vya habari,” alisema Kiganja.

Naye mjumbe wa BMT na Mwenyekiti wa Kamati ya Nidhamu, usuluhishi na Rufaa ya baraza hilo yenye dhamana ya kusimamia chaguzi zote za vyama vya michezo, Jamal Rwambow alimweleza Gidabuday kuhusu kauli zake ngumu alizowahi kuzitoa awali.
jamal
“Katibu Mkuu mpya uliwahi kusema kuwa RT wasiporudi na medali ungefanya nini !!! sasa kama ulivyokuwa ukiisuta RT ukiwa bado hujaikamata nafasi hiyo watu wamekurudisha kundini wana matumaini makubwa kwako,” alisema na kuongeza:

“Kipindi mlichopata cha miaka minne ni kifupi sana, hatutarajii kuona migogoro bali tunarajia kuona timu inatengenezwa vizuri ili kuleta heshima ya Tanzania,” alisema Rwambow.
wote

 

70 total views, 2 views today

Fuatilia Mchezo, like:
0

Leave a Reply

Michezo ni yetu wote, fuatilia, Wataarifu wengi

Follow by Email14
Facebook
Facebook
YouTube0
YouTube
Google+0
Google+
http://nationalsportscouncil.go.tz/blog/2016/11/28/bmt-lafanikiwa-kusimamia-uchaguzi-wa-rt-kwa-amani/">
RSS