WAATALAMU WA MICHEZO ANDIKENI VITABU VYA TAALUMA MBALIMBALI ZA TASNIA HII

Desemba 21                     

Rai hiyo imetolewa  na Mgeni rasmi Mjumbe wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Bibi Jenifer Mmasi Shang’a  wakati wa kuzindua Vitabu vya Soka  vyenye ujumbe wa “BORESHA NA ENDELEZA KIPAJI CHAKO CHA SOKA” vilivyoandikwa na Bw. Gambolii Juma Kimaya hafla iliyofanyika leo uwanja wa Taifa  jijini Dar es salaam.

Jenifer alieleza kuwa,  katika tasnia ya michezo ni ukweli  usiopingika  kuwa  kuna upungufu  mkubwa  wa vitabu vya  Kiswahili katika maktaba zetu,  vilivyopo vipo katika lugha ya kiingereza  ambavyo ni wachache wanaoweza kuvitumia.

“Soka ni mchezo  unaopendwa sana  nchini  na duniani kote  na umechangia kwa kiasi kikubwa  katika maendeleo ya  nchi  kiuchumi, kisiasa na kijamii, hivyo nawashauri  wataalam  kujitokeza  kuandika vitabu kwa wingi vitakavyokuwa msaaada mkubwa kwa walimu wa soka na jamii kwa ujumla,”na kuongeza kuwa:

“Maendeleo ya soka nchini yanakabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo miundombinu mibovu na upungufu wa wataalamu wa kufundisha soka kuanzia ngazi za chini, ili kuleta maendeleo zaidi ya tasnia  hii nchini inahitajika dhamira ya pamoja ya wadau mbalimbali kushirikiana ili kueneza taaluma hii haraka katika jamii pamoja na kujenga misingi imara katika vizazi vya sasa na vijavyo,”alisisitiza Shang’a.

ktb2

Aliendelea kuwa, vitabu alivyoandika Juma  vimesheheni miongozo ya kitaamu inayotoa maarifa ya historia na ufundi wa kisayansi katika soka hivyo vitasaidia  kwa kiasi kikubwa katika kufundishia na kujifunzia, lakini pia vinaelekeza  mazoezi ya viungo ambapo, vikitumiwa vyema na watanzania afya zitaimarika.

Aidha, Jenifer ametoa wito kwa makampuni , taasisi pamoja na wadau kujitokeza  kumsaidia Juma katika kugharamia uchapaji na usambazaji wa vitabu ili elimu hii iweze kuwafikia wengi, vilevile wananchi na shule zinazofundisha michezo kununua vitabu hivyo mara tu vitakapokuwa sokoni.

kt4

Hata hivyo ameeleza kuwa, kwa kuwa nchi bado inakabiliwa na upungufu mkubwa wa vitabu na nyaraka nyingine muhimu za michezo ametoa wito kwa makocha, walimu na wataalamu wengine wa michezo kufuata nyayo za Bw. Juma Gambolii kwa kuandika vitabu vya taaluma ya michezo mbalimbali kwa kujikita katika sehemu zote zinazoendana na maendeleo ya michezo.

Awali Mwenyekiti mstaafu wa BMT Kanali mstaafu Iddy Kipingu alieleza kuwa, wachezaji hawana nadharia ya mchezo husika kitu ambacho kinasababisha makocha  kutumia nguvu kufundisha.

Hata hivyo Kanali Kipingu ametoa wito kwa wataalam kuandika vitabu vingi ili wachezaji wawe na na uelewa kwa kukaa darasani.

“Kijana ametusaidia wapenzi wa soka kwa mchango alioutoa, tunahitaji kujipanga kwa kauli zetu na vitendo vyetu, chanda chema huvikwa pete, tuendelee kumsaidia kijana huyu kwa kujitolea” alisema Kipingu.

Kitabu cha “BORESHA NA ENDELEZA KIPAJI CHAKO CHA SOKA” kimetengwa katika vitabu vinne kulingana na umri, kuanzia miaka 6-14, 14-17, 17-20 na 6-20.

ktb3

66 total views, 1 views today

Fuatilia Mchezo, like:
0

Leave a Reply

Michezo ni yetu wote, fuatilia, Wataarifu wengi

Follow by Email14
Facebook
Facebook
YouTube0
YouTube
Google+0
Google+
http://nationalsportscouncil.go.tz/blog/2016/12/21/waatalamu-wa-michezo-andikeni-vitabu-vya-taaluma-mbalimbali-za-tasnia-hii/">
RSS