SERIKALI YAHAMASISHA USHIRIKI WA WANAWAKE KATIKA MICHEZO

Januari 6,2017
Serikali kupitia Baraza la Michezo la Taifa (BMT) kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa michezo wakiwemo chama cha michezo kwa wanawake (TAWSA)wameendelea kuhamasisha ushiriki wa wasichana na wanawake katika michezo kwenye ngazi na Nyanja mbalimbali zikiwemo Uchezaji, Uamuzi, Ufundishaji/Ukocha, Uongozi/Utawala, Udaktari wa michezo Uwekezaji pamoja na Uwezeshaji, ghafla iliyofanyika leo jijini Dar es salaam.
Aidha, pamoja na juhudi zinazofanywa na wadau mbalimbali za kukuza na kuhamasisha ushiriki wao, bado kuna changamoto ya kuwa na idadi ndogo ya wanawake kutokuwa na fursa ya shiriki katika michezo pamoja na kushindwa kufikia viwango vinavyohitajika katika mashindano na michezo mbalimbali.
Hata hivyo Serikali kupitia mkutano huo inatoa rai kwa jamii kuungana kuhamasisha ushiriki wa wanawake katika michezo kwa Nyanja mbalimbali.
Wadau waliohudhuria katika mkutano huo wameeleza kuwa utakuwa ni mwendelelezo wa vikao vingine vingi kuhakikisha wanafanikiwa wanawake kushiriki katika michezo.

 

kganjaaaa1
Katibu Mkuu wa Baraza la michezo la Taifa (BMT) Bw. Mohamed Kiganja akieleza jambo kwa Waandishi wa habari na wadau wa michezo hawapo katika picha wakati wa mkutano nao wa uhamasishaji wa Wanawake kushiriki katika michezo tarehe 6 Januari, 2017 jijini Dar es salaam.

Mkutano huo ulihusisha Katibu Mkuu wa Baraza Bw. Mohamed Kiganja, wadau wa michezo akiwemo Juliana Yassoda, Mwenyekiti Chama cha wanawake cha mpira wa miguu (TAWFA) Amina Kaluma na Makamu wake Rose Kisiwa, Mhadhiri wa elimu ya michezo UDSM Dr. Devotta Marwa, Ingrid Kimario, Makamu Mwenyekiti Chaneta Bibi Zainabu Mbiro, Maafisa michezo BMT Halima Bushiri, Apansia Lema na Afisa habari Najaha Bakari.

yy
Katibu Mkuu wa Baraza la michezo la Taifa (BMT) Bw. Mohamed Kiganja (kushoto) akisisitiza jambo kwa Waandishi wa habari (hawapo pichani), Wadau wa michezo Juliana Yassoda (katikati) na Amina Karuma (kulia)wakifuatilia kwa makini maelezo ya Katibu.

 

 

84 total views, 1 views today

Fuatilia Mchezo, like:
0

Leave a Reply

Michezo ni yetu wote, fuatilia, Wataarifu wengi

Follow by Email14
Facebook
Facebook
YouTube0
YouTube
Google+0
Google+
http://nationalsportscouncil.go.tz/blog/2017/01/06/serikali-yahamasisha-ushiriki-wa-wanawake-katika-michezo/">
RSS