BMT WAKUTANA NA KAMATI TENDAJI ZA VYAMA KUPANGA MIKAKATI YA USHIRIKI MASHINDANO YA KIMATAIFA

Baraza la Michezo la Taifa (BMT) wamekutana na kamati tendaji za vyama ikiwemo  Kamati ya Olimpiki (TOC) pamoja na Kamati tendaji za vyama vya michezo vinavyoshiriki michezo ya kimataifa kupanga mikakati ya jinsi ya kushiriki katika mashindano hayo ikiwemo michezo ya  jumuiya ya madola (CW),  nchi huru za kiafrika (AAG) na Olimpiki, kikao kilichofanyika jana katika  Ukumbi wa uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

kikaooo
Wajumbe wa kamati tendaji wa vyama mbalimbali vya michezo wakifuatilia kikao kwa makini.

Katika kikao hicho Katibu Mkuu wa Baraza Bw. Mohamed Kiganja amevitaka Vyama hivyo kuwasilisha Mipango kazi yao ifikapo Januari 24 kwa  Baraza na TOC ili kwa pamoja waifanyie kazi na kuona namna ya kuvisaidia vyama ili kufanya vyema katika mashindano ya kimataifa.

1.Katibu Mkuu wa Baraza la michezo la Taifa (BMT) Bw. Mohamed Kiganja (aliyesimama) akifafanua jambo kwa Kamati tendaji za vyama wakati wa kikao chao kuhusu maandalizi ya ushiriki wao katika mashindano mbalimbali ya kimataifa,Mjumbe na Mwenyekiti wa kamati ya nidhamu, usuluhishi na rufaa ya Baraza Bw. Jamal Rwambow (kushoto)  na Mjumbe wa Baraza Bibi. Jennifer M. Shang’a  (kulia),kikao kilichofanyika tarehe 10 Januari, 2017 jijini Dar es salaam
1. Katibu Mkuu wa Baraza la michezo la Taifa (BMT) Bw. Mohamed Kiganja (aliyesimama) akifafanua jambo kwa Kamati tendaji za vyama wakati wa kikao chao kuhusu maandalizi ya ushiriki wao katika mashindano mbalimbali ya kimataifa,Mjumbe na Mwenyekiti wa kamati ya nidhamu, usuluhishi na rufaa ya Baraza Bw. Jamal Rwambow (kushoto) na Mjumbe wa Baraza Bibi. Jennifer M. Shang’a (kulia),kikao kilichofanyika tarehe 10 Januari, 2017 jijini Dar es salaam

“Lengo la Serikali ni kuona vyama vyote vya michezo vinatoka hapa vilipo na  kuleta sifa kwa Taifa vinaposhiriki katika mashindano ya kimataifa kwa kufanya vizuri,”alisema Kiganja.

Kiganja pia ameitaka Kamati ya Olimpiki (TOC) kuunda Kamati za ufundi itakayo shirikisha wataalamu kutoka michezo tofauti ambayo itasaidia kuchagua wachezaji mahiri na wenye viwango watakaoiwakilisha nchi vizuri katika mashindano ya kitaifa na kimataifa.

Aidha,  Kiganja amevieleza vyama kuwa milango ya Baraza iko wazi muda wote wa kazi kwa chama chochote chenye tatizo kufika na kupatiwa huduma  badala ya kutumia vyombo vya habari kusemea mambo yao.

“Lakini pia tumieni katiba zenu kutatua migogoro  na mvitumie vyombo vya habari kueleza maendeleo ya michezo siyo migogoro ndani ya vyama,”alisisitiza.

Mjumbe na Mwenyekiti wa kamati ya nidhamu, usuluhishi na rufaa ya Baraza Bw. Jamal Rwambow akieleza jambo kwa kamati tendaji za vyama katika kikao kilichoandliwa na Baraza tarehe 10 Januari,  kulia ni Katibu Mkuu wa BMT Bw. Mohamed Kiganja.
Mjumbe na Mwenyekiti wa kamati ya nidhamu, usuluhishi na rufaa ya Baraza Bw. Jamal Rwambow akieleza jambo kwa kamati tendaji za vyama katika kikao kilichoandliwa na Baraza tarehe 10 Januari, kulia ni Katibu Mkuu wa BMT Bw. Mohamed Kiganja.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya nidhamu, usuluhishi na rufaa, Bw. Jamali Rwambow  amewataka viongozi  wa vyama  kuheshimu Katiba zao zikiwemo taratibu za kupata viongozi na kuongeza kuwa :

Wagombea wa nafasi mbalimbali za uongozi kuacha kuchukua nafasi kwa ajili ya kujinufaisha badala ya kuhudumia chama kiweze kuwa maendeleo mazuri ya mchezo husika.

Hata hivyo Vyama na viongozi wao wametakiwa kuwa na umoja na ushirikiano ili michezo nchini iweze kuwa na maendeleo na kuleta sifa kwa Taifa.

Mkutano huo ulihusisha Katibu Mkuu wa BMT Bw. Mohamed Kiganja, Kamati ya nidhamu, Usuluhishi na rufaa ya Baraza akiwemo Jamal Rwambow,  Zainabu Mbiro , Mjumbe wa BMT Jenifer Mmasi pamoja na sekretarieti ya Baraza.

Kamati tendaji za Vyama vya michezo zilizoshiriki ni  Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC),  Kamati tendaji ya Shirikisho la ngumi Tanzania (TBF), TAIKWONDO, mchezo wa kuogelea (TSA), Judo (JATA), mieleka (AWATA), baiskeli (CHABATA), mpira wa meza (TTTA) na  riadha (RT).

Wajumbe wa Kamati tendaji za vyama vilivyoshiriki katika kikao hicho.
Wajumbe wa Kamati tendaji za vyama vilivyoshiriki katika kikao hicho.

74 total views, 2 views today

Fuatilia Mchezo, like:
0

Leave a Reply

Michezo ni yetu wote, fuatilia, Wataarifu wengi

Follow by Email14
Facebook
Facebook
YouTube0
YouTube
Google+0
Google+
http://nationalsportscouncil.go.tz/blog/2017/01/11/bmt-wakutana-na-kamati-tendaji-za-vyama-kupanga-mikakati-ya-ushiriki-mashindano-ya-kimataifa/">
RSS