SERIKALI YAWATAKA WANAMICHEZO KUUTEKELEZA MKATABA WA KIMATAIFA WA KUTOTUMIA DAWA NA MBINU ZA KUONGEZA NGUVU MICHEZONI.

Januari 13, 2017

Serikali imewataka Wanamichezo nchini kuutekeleza mkataba wa kimataifa wa kutotumia dawa na mbinu za kuongeza nguvu michezoni ili kupata ushindi wa haki katika mashindano ya Kitaifa na Kimataifa.

Rai hiyo imetolewa leo na Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye katika hotuba yake  iliyosomwa  na katibu Mkuu wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Bw. Mohamed Kiganja katika ufunguzi wa semina ya viongozi wa vyama na Mkocha na wadau michezo iliyoratibiwa na Tume ya Taifa ya ‘UNESCO’ kwa ushirikiano na Wizara yenye dhamana yenye lengo la kutoa uelewa  kuhusu Mkataba wa kimataifa wa udhibiti wa dawa na mbinu za kuongeza nguvu michezoni warsha iliyofanyika leo jijini Dar es salaam.

Bw. Mohamed Kiganja ameongeza kuwa ili kufanikisha maendeleo ya michezo nchini yako mambo muhimu ya kuzingatia ili kudhibiti na kuzuia matumizi ya dawa na mbinu za kuongeza nguvu michezoni.

wadau2
Wadau wa michezo wakifatilia semina kwa makini

Aliendelea kwa kutaja mambo hayo kuwa ni,  elimu kutolewa kwa wanamichezo kuhusu athari ya utumiaji wa dawa na mbinu za kuongeza nguvu michezoni pamoja  na utoaji wa adhabu kali kwa watakaobainika kufanya udanganyifu huo michezoni.

“Ushindi wowote unaopatikana baada ya mchezaji kutumia dawa ama mbinu nyingine yoyote chafu mbali ya kutokuwa haramu lakini pia inamnyima ushindi yule mchezaji ambaye hatumii dawa na inapelekea kutokuwepo kwa ushindani wa haki miongoni mwa wanamichezo wengi” alisistiza Bw. Kiganja.

Awali  Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya UNESCO nchini Dkt. Moshi Kimizi ameeleza kuwa, lengo la semina hiyo ni kutoa mafunzo kwa viongozi wa michezo ambao watasaidia kuipeleka elimu hiyo kwa wanamichezo walio chini ya vyama vyao.

Hata hivyo ameishauri  Serikali kupitia Wizara yenye dhamana ya michezo kuendelea kushirikiana na wadau ili kupata Sheria itakayoendana na mkataba huo wa kimataifa ili kuiendeleza sekta ya michezo kwa manufaa ya wanamichezo na taifa kwa ujumla.

“Niiombe Serikali kupitia Wizara yenye dhamana ya michezo kuendelea kushirikiana na wadau wa michezo na wanamichezo kudhibiti matumizi ya dawa za kuongeza nguvu michezoni ili kulinda heshima ya michezo na taifa kwa ujumla,” alisisitiza Dkt Kimizi.

nkenyenge

Kwa upande wao viongozi na wadau wa michezo wameeleza kufurahishwa sana kupata mafunzo hayo na kuahidi kuyatekeleza ipasavyo ili wasilete aibu kwa Taifa pindi mchezaji wao atakapopatikana na utumiaji wa dawa au mbinu za kuongeza nguvu michezoni katika mashindano mbalimbali.

Semina  hiyo iliyoandaliwa na Tume ya Taifa ya ‘UNESCO’ kwa kushirikiana na Wizara ya Habari utamaduni Sanaa na Michezo yenye lengo la kutoa mafunzo ya siku moja kwa wadau, walimu na viongozi wa vyama vya michezo nchini kuhusu madhara ya matumizi ya dawa na mbinu za kuongeza nguvu michezoni imehusisha takriban washiriki 100 kutoka maeneo mbalimbali nchini.

wadau wa michezo

30 total views, 1 views today

Fuatilia Mchezo, like:
0

Leave a Reply

Michezo ni yetu wote, fuatilia, Wataarifu wengi

Follow by Email14
Facebook
Facebook
YouTube0
YouTube
Google+0
Google+
http://nationalsportscouncil.go.tz/blog/2017/01/13/serikali-yawataka-wanamichezo-kuutekeleza-mkataba-wa-kimataifa-wa-kutotumia-dawa-na-mbinu-za-kuongeza-nguvu-michezoni/">
RSS