BMT WAWAITA TTA KUPANGA TARATIBU ZA UCHAGUZI

Januari 18, 2017

Baraza la michezo la taifa (BMT) wamewaita na kufanya mazungumzo nao Viongozi wa chama cha Tenisi Tanzania kupanga taratibu za uchaguzi mkuu wao, tukio lilifanyika leo katika Ofisi za Baraza jijini Dar es salaam.

Tukio hilo limefanyika baada ya Baraza kuwaagiza viongozi waliobaki katika chama hicho kufanya uhakiki wa wanachama wao kabla ya uchaguzi.

Hata hivyo, katika mazungumzo yao wameafikiana uchaguzi ufanyike tarehe 11 februari 2017, hii ni baada ya kuridhishwa na ukamilishwaji wa kazi ya kuhakiki wanachama ambayo imefanywa na viongozi wanaobaki katika chama baada ya baadhi yao kujiuzulu akiwemo Mwenyekiti Metucela Mbanjo.

Afisa Michezo anayeratibu chama hicho Apansia Lema amesema, maamuzi ya kutangazwa kwa mchakato wa uchaguzi wa TTA umechukuliwa baada ya kikao maalum kilichokaa Octoba 28, 2016 na kuagizwa kufanya uhakiki huo, ambapo mpaka hivi sasa ni mikoa kumi tu ambayo imekamilisha uhakiki kulingana na vigezo vilivyohitajika.

“Sisi kama Baraza tayari kila kitu kimekaa sawa isipo kuwa ni wa tu wa upande wa chama, lakini ni imani yetu kuwa mara baada ya kukutana nao tena kila kitu kitakwenda sawa,”alisema Lema.

Aidha, amewaasa viongozi wanatarajia kuingia kwenye mchakato wa kugombea nafasi za uongozi katika uchaguzi huo, kutotegemea ruzuku kutoka Serikalini bali kuandika maandiko mbalimbali kwa makampuni ili kupata fedha za kuendesha chama.

Amesema ingawa fedha ndio inaonekana kuwa tatizo kubwa katika mchakato huo, amewahamisha kuhakikisha mikoa iliyobakia wanajitahidi kukamilisha uhakiki kwa mikoa iliyobakia.

Uchaguzi huo unatarajia kufanyika Februari 11 mwaka huu huku zoezi la kuchukua fomu likitarajiwa kuanza tarehe 23 januari na kukamilika tarehe 6 Februari wakati tarehe 9 ya mwezi huo utafanyika usahili kabla ya siku ya uchaguzi.

 

109 total views, 1 views today

Fuatilia Mchezo, like:
0

Leave a Reply

Michezo ni yetu wote, fuatilia, Wataarifu wengi

Follow by Email14
Facebook
Facebook
YouTube0
YouTube
Google+0
Google+
http://nationalsportscouncil.go.tz/blog/2017/01/18/bmt-wawaita-tta-kupanga-taratibu-za-uchaguzi/">
RSS