BAWAZIR: NI JUKUMU LENU KUSIMAMIA MCHEZO NA KUUWEKA KATIKA HALI NZURI

13 Februari, 2017

Mwenyekiti wa uchaguzi na Mjumbe wa Baraza la michezo la Taifa (BMT) Bw. Mohamed Bawazir amewataka Viongozi wapya wa Chama cha Tenisi Tanzania (TTA) kusimamia mchezo huo na kuuweka katika hali nzuri ya kuliletea sifa Taifa katika mashindano tofauti.

Rai hiyo ameitoa baada ya kutangaza matokeo ya  uchaguzi wa chama hicho uliosimamiwa na Baraza mwisho wa wiki katika ukumbi wa Uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam.

tenisi bawaziri

“Baraza hatutakuwa wapole tutakapoona viongozi mnashindwa kusimamia mchezo na kuendelea kushuka kiwango badala ya kufanya vizuri katika mashindano mbalimbali ya Kitaifa na Kimataifa,”alisema Bawazir.

Aliongeza kuwa, Viongozi hao hawana budi kuhakikisha wanatekeleza majukumu yao kulingana na Katiba ya chama.

Awali, Kaimu Katibu Mkuu Bw. Milende Mahona amewataka viongozi hao wapya wa TTA kufanya kazi na Baraza na kuacha kufanya kazi kwa mazoea.

Aidha Mahona ameitaka Kamati hiyo mpya ya utendaji kufanya kazi kwa ushirikiano na kuacha kutengana katika kutekeleza majukumu ya chama ili kuleta taswira chanya kwa wadau na Taifa kwa ujumla.

“Fanyeni kazi kwa kushirikiana, kwani umoja ni nguvu,” alisema.

Katika hatua nyingine Rais wa TTA Bw. Dennis Makoi amelihakikishia Baraza  kuwa, Kamati yake itafanya kazi kwa pamoja na kuwatumia wale wote watakaosaidia kuendeleza mchezo huo ili kurudisha hadhi ya tenisi Tanzania.

Katika uchaguzi huo viongozi walichaguliwa ni Rais Bw. Dennis S. Makoi, Makamu wa Rais Bw. John Bura, Katibu Mkuu Bi. Irene J. Mwasanga,  Wajumbe ni Rehema A. Mbegu, Riziki S. Seleman, Mosses Mabura na Sanjay A. Chokshi.

Hata hivyo Baraza nimewaagiza viongozi hao kuhakikisha ndani ya miezi mitatu (3) kuanzia siku ya uchaguzi kuandaa uchaguzi mdogo ili kujaza nafasi zilizoachwa wazi ikiwemo ya Katibu Mkuu msaidizi na Mweka hazina.

tenisi4
Kamati mpya ya Utendaji ya chama cha tenisi Tanzani (TTA) wakiwa katika picha ya pamoja baada ya uchaguzi uliofanyika tarehe 11 Februari, 2017 jijini Dar es salaam.

71 total views, 2 views today

Fuatilia Mchezo, like:
0

Leave a Reply

Michezo ni yetu wote, fuatilia, Wataarifu wengi

Follow by Email14
Facebook
Facebook
YouTube0
YouTube
Google+0
Google+
http://nationalsportscouncil.go.tz/blog/2017/02/13/bawazir-ni-jukumu-lenu-kusimamia-mchezo-na-kuuweka-katika-hali-nzuri/">
RSS