SERIKALI  YAWATAKA  WANAMICHEZO  KUTAFUTA  USHINDI  WA HAKI

Februari 18, 2017

Naibu Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Anastazia Wambura amewataka wanamichezo nchini kuongeza juhudi ya kufanya mazoezi ili wapate ushindi wa haki katika mashindano mbalimbali.

16804470_1272974502788807_303696325418610382_o
Naibu Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Anastazia Wambura akieleza jambo kwa Wanafunzi na wadau waliohudhuria katika tamasha hilo mwisho wa wiki

Rai hiyo ameitoa leo  wakati wa tamasha la kupinga matumizi ya dawa na mbinu za kuongeza nguvu michezoni lililofanyika katika uwanja wa uhuru na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wa michezo nchini, zikiwemo na shule  5 za msingi na 5 sekondari za Manispaa ya Temeke jijini Dar es salaam.

Amesema kitendo cha mchezaji kutumia dawa  za kuongeza nguvu michezoni ni kinyume na Sheria pamoja na taratibu za nchi na kudai kuwa watu wa namna hiyo wamekuwa wakisababisha kutokuwepo kwa ushindani  wa haki katika sekta ya michezo.
SAYNO
Aliongeza kuwa,  kuwepo kwa ongezeko la watumiaji wa dawa na mbinu za kuongeza nguvu michezoni, kupitia Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni(UNESCO)waliandaa mkataba maalum ambao kila mwanachama wa shirika hilo alipaswa kuridhia na kutia saini mkataba huo wa kupambana na kuzuia matumizi ya dawa za kuongeza nguvu.

Alieleza  kuwa,  kwa bahati mbaya Tanzania ilichelewa kuridhia mkataba huo kwa sababu mbalimbali walizokuwa wakizifahamu lakini Serikali ya awamu ya tano iliona umuhimu wa kuridhia mkataba huo mwezi June mwaka jana.
kwa ajili ya maendeleo ya michezo hapa nchini.

antdopin magunia

“Leo hii tumekutana kwenye hili Tamasha ambalo limeandaliwa na UNESCO kwa Ushirikiano na Baraza la Michezo la Taifa(BMT) ili tuweze kuelekezana madhara ya matumizi ya dawa na mbinu za kuongeza Nguvu michezoni kwa sababu tumekuwa tukizidi kupunguza ushindani kila siku kutokana na kuendekeza matumizi haya ya dawa, na niwatake wananchi kuungana kwa pamoja kupinga suala hili,” amesema.Wambura

Aliendelea kuwa,  adhabu zinazotolewa kwa watu wanaotumia dawa na mbinu za kuongeza nguvu michezoni ni pamoja na kupokonywa ushindi pamoja na mataji mbalimbali ambayo watakuwa wameyatwaa na kuongeza kuwa hawatakubali adhabu kama hizo ziwakute timu zetu za Taifa zinazoshiriki michuano mbalimbali.
mah
Pia Wambura amewataka watanzania kujenga desturi ya kufanya mazoezi ya viungo kwani kwa kufanya hivyo magonjwa yasiyo ya kuambukizwa ambayo yamekuwa yakilisumbua taifa kwa muda mrefu, yatapungua na kwisha kabisa.

mrope

Kwa Upande wake Naibu Katibu Mtendaji wa Tume ya UNESCO, Fatma Mlope amesema wanachotakiwa kufanya wanamichezo wa Tanzania ni kutekeleza matakwa ya mkataba huo ili kujiweka katika mazingira mazuri ya kimichezo kitaifa na kimataifa.

Katika kuhakikisha hilo linatimia amesema anaimani Wizara yenye dhamana ya michezo kwa kushirikiana na wadau
mbalimbali wa michezo nchini watafanikisha uundwaji wa Sheria za kitaifa za kudhibiti mbinu na matumizi ya dawa za kuongeza nguvu michezoni ili kuwezesha usimamizi na utekelezaji wa mkataba huo.

“Mkataba huu uliopitishwa na bunge la jamhuri ya Muungano Tanzania mwezi Juni mwaka 2016, unamalengo ya kuona wanamichezo wa hapa nchini na duniani kiujumla wanatumia uwezo wao binafsi kupata ushindi na sio njia haramu ambazo zimekuwa zikizidi kurudisha nyuma maendeleo ya sekta ya michezo kila siku zinavyozidi kwenda mbele,”amesema Mlope.

antdopin 5

Tamasha hilo lilianza kwa matembezi ya km 5 majira ya saa 12 asubuhi, mazoezi ya viongo na kufuatiwa na michezo mbalimbali iliyonogeshwa na wanafunzi wa shule za msingi na sekondari za Manispaa ya Temeke.

antdopin3

 

 

49 total views, 2 views today

Fuatilia Mchezo, like:
0

Leave a Reply

Michezo ni yetu wote, fuatilia, Wataarifu wengi

Follow by Email14
Facebook
Facebook
YouTube0
YouTube
Google+0
Google+
http://nationalsportscouncil.go.tz/blog/2017/02/20/serikali-yawataka-wanamichezo-kutafuta-ushindi-wa-haki/">
RSS