MHESHIMIWA WAMBURA AVITAKA VYAMA VYA MICHEZO KUPATA BARAKA ZA SERIKALI KABLA YA KWENDA KATIKA MASHINDANO YOYOTE.

10 Marchi, 2017
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mheshimiwa Annastazia Wambura amevitaka Vyama vya mchezo kuhakikisha wanapata baraka za Serikali kwa kupata kibali na Bendera vinaposhiriki katika mashindano yoyote nje ya nchi.
Hayo ameyasema jana alipokuwa anapokea Kombe la ushindi kutoka kwa wachezaji wa tenisi kwa watu wenye ulemavu (wheelchair tennis) walilotwaa katika mashindano ya Afrika yaliyomalizika mwishoni mwa mwezi Februari nchini Nairobi Kenya.

wambura2 (1)
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mheshimiwa Annastazia Wambura (nguo nyekundu) akifuatiwa na Mkurugenzi wa michezo kulia Bw. Yusuph Singo wakiwa katika picha ya pamoja na Vionozi wa TTA na wachezaji wa tenisi watu wenye ulemavu.


“Hongereni kwa kuleta sifa kwa Taifa ila imekuwa kama mshangao Serikali kutokuwa na taarifa ya safari yenu katika mashindano hayo,”alisema Mhe. Wambura.
Katika mashindano hayo Tanzania imeibuka mshindi wa kwanza na kutawazwa mwakilishi wa Bara la Afrika katika mashindano ya Dunia yanayotarajiwa kufanyika mjini Sardinia nchini Italy kuanzia tarehe 1 hadi 7 mwezi Mei mwaka huu.
Timu za Tanzania Wanawake na Wanaume wamefuzu katika mashindano hayo baada ya kuziburuza timu kutoka nchi 6 shiriki katika mashindano hayo ikiwemo Morocco, Nigeria, Egypty, Gambia, Ghana na mwenyeji wa mashindano Kenya.
Katika hatua nyingine, Mkurugenzi wa maendeleo ya Michezo Bw. Yusuph O. Singo amewapongeza sana na kuwashauri kuacha kushiriki mashindano mbalimbali ya nje bila Serikali kuwa na taarifa.
Kwa upande wake Rais wa chama cha Tenisi Tanzania (TTA) ameiomba Serikali kuwasaidia wachezaji hao kupata sehemu ya kufanyia mazoezi kwakuwa hiyo ni changamoto inayowakumba pamoja na kufanya vyema wanaposhiriki mashindano mbalimbali.
Wachezaji walioipa sifa nchi katika mashindano hayo kwa upande wa wanaume ni Novatus Temba, Juma Hamis na Jumanne Nassoro na timu ya Wanawake iliwakilishwa na Rehema Selemani na Luce Julius wakiwa chini ya uongozi wa Kocha wao Riziki Salum.

34 total views, 1 views today

Fuatilia Mchezo, like:
0

Leave a Reply

Michezo ni yetu wote, fuatilia, Wataarifu wengi

Follow by Email14
Facebook
Facebook
YouTube0
YouTube
Google+0
Google+
http://nationalsportscouncil.go.tz/blog/2017/03/10/mheshimiwa-wambura-avitaka-vyama-vya-michezo-kupata-baraka-za-serikali-kabla-ya-kwenda-katika-mashindano-yoyote/">
RSS