BMT YAHAKIKISHA CHAMA CHA MASHUA TANZANIA(TSSA) WANAKUA NA VIONGOZI WA KUCHAGULIWA.

Baraza la michezo Taifa limeratibu na kusimamia uchaguzi wa Chama cha Mashua Tanzania ambao haujawahi kufanyika karibu miaka kumi iliyopita. Uchaguzi huo umefanyika leo katika ukumbi wa uwanja wa uhuru  jijini Dar es salaam.

Mwenyekiti wa uchaguzi kutoka katika kamati ya nidhamu ,usuluhishi  na rufaa kamanda mstaafu Jamal Rwambow amewataka viongozi waliochaguliwa  katika uchaguzi huo kuhakikisha wanafuata sheria ya Baraza  kwa kufanya chaguzi kwa wakati.

wajumbe

“sheria ya Baraza la Michezo lazima muiheshimu na kuhakikisha       mnafanya chaguzi kwa wakati”alisema Rwambow

Nafasi ya Mwenyekiti imechukuliwa na Philimon Nassari mgombea pekee aliye aliye jinyakulia kura 31 kati ya 32, huku nafasi ya katibu mkuu ikienda kwa Nelly Coelch aliye jinyakulia kura zote 32 akiwa mgombea pekee.

Kwa upande ya nafai ya Mweka hazina imebaki wazi kwa kuwa mgombea hakuwa mtanzania.

Huku nafasi ya Ujumbe ikichukuliwa na Halide Mponda kwa kura 25,Joyce  Makunde kura 21, Vincent Kulagwa kura 21 na Jamal Hamis mwenye kura 18 ambapo wajumbe walitakiwa wanne.

Hata hivyo Mwenyekiti  wa uchaguzi amewataka viongozi wapya wa Chama cha Mashua  kuhakikisha ndani ya siku 90 baada ya uchaguzi wanafanya uchaguzi mdogo ili kujaza nafasi iliyoachwa wazi.

 

sailing 3

Kwa upande wake Kaimu Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo Milinde Mahona  ameeleza kuwa wadau  ambao siyo raia wa Tanzania tunafanya nao kazi lakini isiwe kwenye uongozi hususani katika nafasi za juu.

“Tunafanya kazi na wadau wananchi nyingine katika nyanja tofauti lakini siyo kuongoza  tena katika nafasi za juu.

Naye Mwenyekiti mpya TSSA Philimon Nassari ameahidi kufanya   kazi kwa kufuata sheria ya BMT na kuhakikisha anailetea sifa nchi katika mashindano mbalimbali.

sailing2
Uongozi mpya wa Chama cha Mashua 2017

 

47 total views, 1 views today

Fuatilia Mchezo, like:
0

Leave a Reply

Michezo ni yetu wote, fuatilia, Wataarifu wengi

Follow by Email14
Facebook
Facebook
YouTube0
YouTube
Google+0
Google+
http://nationalsportscouncil.go.tz/blog/2017/03/30/bmt-yahakikisha-chama-cha-mashua-tanzaniatssa-wanakua-na-viongozi-wa-kuchaguliwa/">
RSS