PROF. ELISANTE OLE GABRIEL AWAOMBA WAFADHILI KUUNGA MKONO MICHEZO KWA WANAWAKE.

07 Aprili,2017

Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel amewaomba wafadhili kujitoa katika kufadhili michezo ya wanawake ili itambulike na kupata  mafanikio  hapa nchini.

Hayo ameyasema  leo wakati alipokuwa akizindua mkutano wa wanawake na Michezo uliondaliwa na Baraza la Michezo la Taifa (BMT) na kufanyika mwisho wa wiki katika ukumbi wa uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

“Wafadhili mmekua msaada katika maendeleo ya michezo nchini hivyo tunaamini mnaweza kuwa mchango mkubwa katika kuinua michezo kwa wanawake,”alisema.

Prof. Elisante alisema kuwa, michezo inahitaji msaada mkubwa kutoka kwa wafadhili mbalimbali  hivyo ni wajibu wao kuona jitihada zinazooneshwa na wanawake  wanaziunga mkono.

“Michezo ni afya, ni ajira lakini pia inaleta umoja na ushirikiano katika kutafuta maendeleo kwa jamii, nawaomba wadhamini mjitokeze kuunga mkono jitihada hizi,”alisema Katibu Mkuu huyo.

Aidha Katibu Mkuu huyo amewataka viongozi wa vyama vya michezo vya wanawake kuwa wabunifu katika kutafuta fursa zilizopo katika michezo ili waweze kufanikiwa zaidi pamoja na kusimamia yale wanayo yaazimia kwa maendeleo ya Michezo yao na kuongeza kuwa:

“Kujiamini ni jambo muhimu kwa kiongozi na unatakiwa uwe sehemu ya majibu badala ya matatizo, michezo ni sehemu kubwa ya kutatua matatizo.”

IMG_9929
Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel akiwa katika picha ya pamoja na wanawake walioshiriki katika mkutano baada ya uzinduzi.

Katika hatua nyingine, Mjumbe wa Baraza la Michezo la Taifa Bibi Jenifer Mmasi amesema kuwa, kongamano hilo lina lengo la kuwakutanisha wanawake ambao ni wanamichezo kupata ujuzi na namna bora ya kutumia michezo katika jamii zao kama njia ya kutatua changamoto mbalimbali za maendeleo.

“Ni vizuri kwenu viongozi kutumia fursa hii kujifunza zaidi ili mnapokuwa katika maeneo yenu muwaelimishe wanawake wengine umuhimu wa kushiriki katika michezo,”Alisema  Bibi Jenifer.

Kongamano hilo la siku moja linalenga kujadili jinsi wanawake wanavyoweza kufanikiwa kupitia michezo pamoja na changamoto ambazo wanawake wanakutana nazo katika kushiriki michezo  na kuzitafutia  ufumbuzi.

128 total views, 1 views today

Fuatilia Mchezo, like:
0

Leave a Reply

Michezo ni yetu wote, fuatilia, Wataarifu wengi

Follow by Email14
Facebook
Facebook
YouTube0
YouTube
Google+0
Google+
http://nationalsportscouncil.go.tz/blog/2017/04/07/prof-elisante-ole-gabriel-awaomba-wafadhili-kuunga-mkono-michezo-kwa-wanawake/">
RSS