MWAKYEMBE: UKIMWELIMISHA MWANAMKE UMEELIMISHA TAIFA

Aprili 8, 2017

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dr.  Harrison Mwakyembe ameeleza kuwa elimu yoyote ikitolewa kwa mwanamke unakuwa umeelimisha Taifa zima.

Rai hiyo ameitoa wakati wa Tamasha la michezo kwa Wanawake lililoandaliwa na Baraza la michezo la Taifa kwa kushirikiana na wahisani na wadau mbalimbali, tamasha lililofanyika mwisho wa wiki katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam.

1.Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dr. Harrison Mwakyembe akieleza jambo kwa Wanawake (hawapo pichani) wakati wa Tamasha la Wanawake na michezo lililofanyika tarehe 08 Aprili katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam.
1. Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dr. Harrison Mwakyembe akieleza jambo kwa Wanawake (hawapo pichani) wakati wa Tamasha la Wanawake na michezo lililofanyika tarehe 08 Aprili katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam.

“Ukimwelimisha mama umeelimisha jamii,”alisema Mhe. Waziri

Dr. Mwakyembe alieleza kuwa, tamasha hilo lina maana sana kwa nchi na anatamani lingefanyika katika kila Mkoa na Wilaya na kuahidi kulisimamia hilo katika sehemu hizo ili kuhamasisha ushiriki wa wanawake katika michezo.

Aliendelea kuwa, mwaka huu mashindano ya michezo shule za Msingi na Sekondari (UMISETA  na UMITASHUMTA) yatafanyika ili kuendelea kuibua vipaji kutoka ngazi za chini na kuleta mafanikio mazuri katika ngazi ya Taifa kwa jinsia zote.

5
Wanawake wakiwa katika matembezi wakati wa Tamasha la Wanawake na michezo mwishoni mwa wiki jijini Dar es salaam.

“Mwaka jana mashindano ya Umiseta na Umitashumta yalisimamishwa na Mhe. Rais kutokana na sababu ambazo zisizozuilika, ila mwaka huu yatafanyika ili tuzidi kuendelee kuibua vipaji kutoka ngazi ya chini,” alisema Dr. Mwakyembe.

“Leo hii tunajivunia vijana wa Serengeti boys na Twiga stars ambao katika michezo mingi ya kimataifa  wamefanya vizuri, hii ni kwakuwa wameandaliwa vizuri kuanzia chini na nitaendelea kuwalea” alieleza Mhe. Mwakyembe.

43
Wanawake wakiwa katika matembezi wakati wa Tamasha la Wanawake na michezo mwishoni mwa wiki jijini Dar es salaam.

Awali, Makamu Mwenyekiti wa BMT Mhe. Zaynab Vulu alisema kuwa, Wizara lazima izingatie  kutoa miundombinu rafiki kwa Wanawake  ili iwe rahisi kwao kushiriki katika michezo kwa wingi.

Aliongeza kuwa, Wazazi wanapokuwa wanashiriki katika michezo inapelekea familia kuishi kwa amani na kupunguza ugomvi ndani ya nyumba.

4.Katibu Mkuu wa BMT Bw. Mohamed Kiganja akishiriki katika mchezo wa kukuna nazi wakati wa Tamasha
4. Katibu Mkuu wa BMT Bw. Mohamed Kiganja akishiriki katika mchezo wa kukuna nazi wakati wa Tamasha

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Temeke Bw. Felix  Lyaviva  Alisema,  michezo inasaidia wananchi kutokwenda hospitali  na kueleza kuwa yeye katika Wilaya yake ameweka utaratibu  kwa Watumishi kila Ijumaa jioni kushiriki katika michezo.

6
Wanawake wakiwa katika matembezi wakati wa Tamasha la Wanawake na michezo mwishoni mwa wiki jijini Dar es salaam.

 

120 total views, 2 views today

Fuatilia Mchezo, like:
0

Leave a Reply

Michezo ni yetu wote, fuatilia, Wataarifu wengi

Follow by Email14
Facebook
Facebook
YouTube0
YouTube
Google+0
Google+
http://nationalsportscouncil.go.tz/blog/2017/04/08/mwakyembe-ukimwelimisha-mwanamke-umeelimisha-taifa/">
RSS