TIMU YA CHESS CHINI YA MIAKA 16 KUONDOKA TAREHE 15 KUELEKEA KENYA

Wachezaji wa mchezo wa chess umri chini ya miaka16 wanatarajia kuondoka tarehe 15 kuelekea Kenya kwenye mashindano ya Afrika kanda ya 4.2 yanayotarajiwa kuanza tarehe 16 hadi 22 Mjini Mombasa.

Tanzania ni mwanachama wa Afrika kanda ya 4.2 ambayo inahusisha nchi 13 zikiwemo Rwanda, Burundi, Uganda, Somalia, Djibouti, Eritrea, Egypt, Seychelles, Ethiopia, South Sudan, Sudan, na mwenyeji wa mashindano Kenya.

Timu ya Tanzania itawakilishwa na wachezaji watano (5) wakiwemo wavulana 3,Cleophas Charles, Shedrack Lusako, na Anacleutus Moras, pamoja na wasichana 2 akiwemo Asha Kondo na Navini Choudary.

Kocha atakaye ongozana na timu hiyo ni Kara Louis akiongozana na Mjumbe wa kamati kuu ya chama cha mchezo wa chess Tanzania.

Wawakilishi wa Tanzania katika mashindano hayo wamepatikana baada ya mchujo uliofanyika kituo cha vijana Don Bosco kuanzia tarehe 8 mpaka 9 Aprili.

Katibu Mkuu wa chama cha Chess Tanzania Nurdin Hassuji katika taarifa yake ametoa matumaini makubwa kwa Watanzania kuwa wachezaji hao watarudi na ushindi kutokana na maandalizi bora waliyopatiwa.

44 total views, 1 views today

Fuatilia Mchezo, like:
0

Leave a Reply

Michezo ni yetu wote, fuatilia, Wataarifu wengi

Follow by Email14
Facebook
Facebook
YouTube0
YouTube
Google+0
Google+
http://nationalsportscouncil.go.tz/blog/2017/04/12/timu-ya-chess-chini-ya-miaka-16-kuondoka-tarehe-15-kuelekea-kenya/">
RSS